WASHTAKIWA MAUAJI LOLIONDO WALIVYOFUTIWA KESI ARUSHA

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 6. 09. 2024
  • Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewafutia kesi Watu 24 Wakazi Wa Ngorongoro wakiwemo Madiwani 10 na Mwenyekiti Wa CCM Mstaafu Ndirango Senge waliokuwa wakikabiliwa na Mashtaka ya mauji ya Askari aliyekuwa akishiriki zoezi ya uwekaji alama za mipaka katika pori Tengefu la Loliondo.
    Uamuzi Wa Mahakama hiyo umekuja baada ya Upande Wa Jamhuri Kuonyesha Nia ya kutokuendelea na Shauri hilo.
    Aliyekuwa mshtakiwa namba moja kwenye Kesi hiyo ni Malongo Pascal ambapo yeye na Wenzake Walidaiwa kupanga Njama na kumuua Askari Polisi, G 4200 Koplo Garlus Mwita Kwa mshale.
    Tukio Hilo lilidaiwa Mahakamani hapo kuwa lilitokea eneo la Selo Ololosokwan Tarafa ya Loliondo Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha mnamo Juni 10, 2022.
    Yalielezwa kuwa makosa hayo ni Kinyume na Kifungu Cha 196 Cha sheria makosa ya adhabu uliiyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.
    Nje ya Mahakama vilio Vya Furaha vilitawala wakati Waliokuwa washtakiwa hao wakitoka, na kupokelewa na Ndugu Jamaa na Marafiki.

Komentáře •