WAZIRI WA ELIMU ATINGA KWENYE SHULE HII ILIYOTIA AIBU KUBWA MWANZA,AZUNGUMZA NA WAZAZI WALIOANDAMANA

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 18. 02. 2023
  • Serikali kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wahusika wote wa shule zilizobainika kufanya udanganyifu wa mitihani ya kidato cha nne 2022
    Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema Serikali inaendelea kufanya uchunguzi kwa shule zote nne zilizobainika kufanya udanganyifu wa mitihani ya kidato cha nne mwaka 2022 na wahusika wote watakao bainika watachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.
    Akizungumza leo kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na wazazi wa wanafunzi 140 wa shule ya Sekondari ya Thaqafa waliofutiwa matokeo yao,Mhe.Mkenda amesema vitendo hivyo havitavumiliwa la kuja kuwa na Taifa la watu wasio na weledi na wasomi wababaishaji.
    Kuhusu ombi la wazazi hao la kutaka watoto wao kurudia mitihani,Waziri Mkenda amesema kwa sasa hawezi kuwa na jibu la moja kwa moja kutokana na suala hilo kuwa la kibajeti zaidi na Baraza la Mitihani la Taifa halina fungu hilo kwa sasa hivyo wampe muda wa kuzungumza na wasaidizi wake Wizarani na baadaye Serikali itakuwa na jibu la kuwapa.
    Aidha amewashauri wazazi wanaowasomesha watoto wao kwenye shule hizo nne ambazo ni Mnemonic ya Zanzibar,Thaqafa kutoka Mwanza,Cornelius ya Dar es Salaam,na Twibhoki kutoka Mara wajitathmini kama watoto wao wanastahili kuendelea kusoma kwenye shule hizo kabla ya hatua za kinidhamu hazijachukuliwa na Serikali.
    "Wazazi wenzangu awali ya yote poleni sana, natambua mlivyo umizwa na jambo hili,Kamishna wa Elimu Dkt.Lyabwene Mutahaba na timu yake wapo katika hatua za uchunguzi kwa shule hizo na hatua itakayofuatia ni kuzifutia usajili ili iwe fundisho kwa wengine wanaojihusisha na mmomonyoko huo wa maadili" Prof.Adolph Mkenda.
    Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Adam Malima amewataka wazazi hao kuwa na subira wakati Serikali inakwenda kulifanyia kazi ombi la watoto wao kupewa nafasi ya kurudia mitihani hiyo.
    "Serikali ya Dkt.Samia Suluhu ni sikivu na inawajali wananchi wake kama mlivyoona Waziri muhusika amefika hapa Mwanza kuja kuwasikiliza ombi lenu,hivyo mpeni muda akakutane na wasaidizi wake Wizarani kuona namna ya kulifanyia kazi"Mkuu wa Mkoa.
    "Mhe.Waziri tunaamimi nawe ni mzazi tumeguswa sana na udanganyifu huu uliofanyika ambao umeingia kutugharimu sisi wazazi, tunakuomba sana utufutie machungu haya kwa kuwaruhusu watoto wetu kurudia mitihani yao" Patrick Masagati Mwenyekiti wa Wazazi

Komentáře • 4

  • @mercypeter162
    @mercypeter162 Před rokem +1

    Poleni sana wazazi. Asante waziri kwa kazi nzuri

  • @kibiritieda9469
    @kibiritieda9469 Před rokem

    Msiangalie shule tu na watoto pia muangalie kwann walikubali kupewa majibu? Makosa yako kwa shule na watoto pia.Aliepewa mkosaji aliepokea mkosaji