Kibonge Wa Yesu - Neno Moja (Official Music Video) SMS Skiza 8021080 to 811

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 28. 02. 2024
  • Mawazo ya mwanadamu wakati Mwingine ni ya kukata tamaa lakini Mungu anaweza kusimama na kauli yake Moja tu inayoweza kubadili hatima ya Mwanadamu na kurejesha vilivyopotea na kuhuwisha vilivyokufa. Wimbo huu ukawe wa Urejesho na uponyaji wa majeraha kwa kila moyo uliyoumizwa na kukosa tumaini Mungu akawe Msaada kwako katika Jina la Yesu. Amen!🙏
    John 5:5-6
    Audio produced by ​⁠‪@kstarrecords255‬
    Video directed by @mrazalia
    Bvg : Nuru mwaipungu
    Get it on ALL DIGITAL PLATFORMS
    Listen to NENO MOJA by Kibonge Wa Yesu
    On Boomplay: www.boomplaymusic.com/share/m...
    On Audiomack: audiomack.com/kibonge-wa-yesu...
    ©2024KiboMelodies.All rights Reserved.
    #kibongewayesu #gospelmusic #NenoMoja #Semanenomoja
    Verse 1
    Kauli yako moja tu inaweza kubadili hatima
    kauli yako inabadilisha mambo
    kauli yako moja inaweza kunitengeneza
    vilivyo kufa kwangu vikachipuka tena
    na nimekuja hapa Mungu na uchumi wangu ulioyumba, afya yangu nafsi yangu uvihuwishe tena
    kuna muda nakubali huenda sababu ni mimi mwenyewe
    ule muda najikwaa kwa kufuata yangu na kukuacha wewe
    uliempa ndege uwezo wa kupaa angani haya matatizo,shida kwako ni kitu gani?
    uliempa samaki uwezo apumue majini haya masimango,mateso ebaba tupilia mbali
    Hook:
    Nikakuomba Mungu nakuomba kama kulia nimelia sana inatosha
    ninakuomba Mungu nakuomba kama kuchekwa nimechekwa sana inatosha
    baba Mungu wangu wee
    .
    Chorus:
    Sema neno Moja
    ninakuomba useme
    nipo tayari kupokea
    kwa neno lako ntapona Yesu
    sema neno moja
    kwa neno lako ntashinda mie
    nipo tayari kupokea
    baba Mungu wangu wee
    sema neno moja
    ninakuomba useme
    nipo tayari kupokea
    kwa neno lako ntapona Yesu
    sema neno moja
    kwa neno lako ntashinda mie
    nipo tayari kupokea
    Verse 2
    kama batimayo nipo kando ya njia
    Ooh Baba
    nakusubiri useme ili nione
    Ooh Baba
    japo nimesikia mengi ya kunikatisha tamaa ila neno lako moja linaweza niinua tena
    Nimeomba sana mpaka wanasema ninapiga kelele
    ila sichoki bado nakazana kukusubiria wewe
    kama kukwama nimekwama
    na kiza kimetanda
    nategemea neno lako nuru liniangazie
    kama msaada sijaona kwa watu wadunia
    nategemea ulie juu unisadie
    hook :
    Nikakuomba Mungu nakuomba kama kulia nimelia sana inatosha
    ninakuomba Mungu nakuomba kama kuchekwa nimechekwa sana inatosha
    baba Mungu wangu wee
    Chorus:
    sema neno moja
    ninaomba useme
    nipo tayari kupokea
    kwa neno lako ntashinda
    sema neno moja
    mhh
    nipo tayari kupokea
    kwa neno lako nitainuka tena
    sema neno moja
    neno la baraka
    nipo tayari kupokea
    neno neno lako
    sema neno moja
    neno la kunitajirisha
    nipo tayari kupokea
    litanipa amani
    neno litanifariji

Komentáře • 562