MAFANIKIO YA WAKULIMA 7,000 | WANAWAKE WANAFIKA 3,000

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 8. 09. 2024
  • Kutoka Kanda ya Nyanda za Juu Kusini tumefanikiwa kuzungumza na Mdau mkubwa kwenye sekta ya kilimo kutoka shirika lisilo la kiserikali la Movement for Community Development - MCODE Tanzania linalofanya kazi na Taasisi ya PASS Trust katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo wa kilimobiashara kupitia vikundi.
    MCODE Tanzania wanajihusisha na kuwasaidia wajasiriamali wadogo kuunda na kusajili vikundi, kuunganisha vikundi na PASS Trust, utoaji wa huduma ya mikopo ya pembejeo, utoaji wa elimu ya ugani, kuunganisha vikundi na taasisi za fedha, kusaidia kuhakiki masoko, utoaji wa mbinu za kupunguza upotevu wa nafaka mara baada ya kuvuna, utoaji wa elimu ya utunzaji wa mazingira n.k. MCODE Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto za wajasiriamali wadogo na kupelekea kuendelea kuongeza maeneo (mikoa) ya kuwahudumia.
    Mpaka sasa, MCODE Tanzania imeshawawezesha wajasiriamali wadogo wa kilimobiashara wapatao zaidi ya 7,000; jambo lililopelekea kutengeneza fursa nyingi sana za ajira za muda mfupi na za muda mrefu kupitia wajasiriamali hawa waliowezeshwa, kuongeza mikoa ya utoaji wa huduma n.k. Pia, wamejipanga kuendelea kutoa elimu na mafunzo ya utekelezaji wa miradi ya kilimo (mnyororo wa thamani) kwa kuzingatia utunzaji wa mazingira, jambo litakalo viwezesha vikundi kupata dhamana ya hadi asilimia 80 ya mkopo wa kilimo kutoka PASS Trust kutokana na kufanya kilimo kinachozingatia utunzaji wa mazingira.
    MCODE Tanzania inaendelea kuwawezesha wajasiriamali wadogo kupitia vikundi kwa ushirikiano mkubwa na PASS Trust, kwani baada ya vikundi hivyo kukamilisha taratibu zote, vimekuwa vikipatiwa mikopo ya pembejeo kutoka benki (washirika wa PASS Trust) kupitia dhamana za PASS Trust. Taasisi ya PASS Trust inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa lengo la kupunguza umaskini kupitia mapinduzi ya kilimobiashara.
    Kwa taarifa zaidi wasiliana na Kituo cha Huduma kwa Wateja: Piga simu bure: 0800 750 037 Jumatatu - Ijumaa, Saa 2:00 asubuhi - saa 11:00 jioni. Tovuti: www.pass.or.tz
    #VIJISTORIVYASHAMBA
    (Media Presenter: Philbert Francis Felix - PASS Trust)
    #vijistorivyashamba #kijanishamaisha #passtrust #passtanzania #passkilimo

Komentáře • 1