Mgomo wafanyabiashara Soko la Mwanjelwa waingia siku ya pili, utitiri wa kodi za TRA watajwa

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 23. 05. 2024
  • Mgomo wa wafanyabiashara katika Soko la Mwanjelwa jijini Mbeya, umeendelea tena leo baada ya maduka kutofunguliwa.
    Mgomo huo ulioanza jana Mei 23, unafanywa na wafanyabiashara wanaodai kuwapo utitiri wa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), manyanyaso, kukamatwa kwa mizigo yao na kufungiwa maduka na Halmashauri ya Jiji la Mbeya pindi wanapochelewesha malipo ya huduma kwa wateja.
    Mwananchi Digital imefika asubuhi ya leo Mei 24, 2024 katika soko hilo kubwa jijini hapa na kushuhudia maduka yakiwa yamefungwa, huku wafanyabiashara wakiwa katika makundi wakiendelea na maongezi binafsi.
    Hata hivyo, habari ambazo hazijawa rasmi kutoka kwa wafanyabiashara, zinaeleza kuwa mgomo huo utadumu kwa siku mbili wakati wakisubiri hatma ya kilio chao kama kitasikika kwa Serikali.
    Mmoja wa wafanyabiashara ambaye hakutaja majina yake, amesema kwa sasa wanasubiri tamko la viongozi wao kujua lini wataanza kutoa huduma.
    "Leo tumeambiwa kutakuwapo na mkutano kwa hiyo tupo hapa tunasubiri huenda viongozi wetu wapo kwenye kikao ili baadaye watuite, hatufungui hadi tutakapopewa maelekezo," amesema.
    Endelea kufuatilia Mwananchi na mitandao yetu kwa habari zaidi.

Komentáře • 5

  • @hurumalunda2490
    @hurumalunda2490 Před měsícem

    Tuendelee tu na biashara aa

  • @judithtitomalyeta4000
    @judithtitomalyeta4000 Před měsícem

    Kachawi nn aka kajamaa tenA katoto hakajui hata kiswahili

  • @hurumalunda2490
    @hurumalunda2490 Před měsícem

    Hakuna mwanafunzi anayesoma ili asaidie watu ila utajiri wake,,hivyo inchi haiwezi kunyooka ,saa ingine inch inataka kuongeza mzunguko ili ikopesheke nje ,, ila watatuua,, 😶😶

  • @MahegaSiyantemi
    @MahegaSiyantemi Před 2 měsíci

    TRA wametinga sana

  • @dorisedom7358
    @dorisedom7358 Před měsícem

    Sio wewe tu mama tra wanatusababishia hata magojwa roho juju Mimi nasuka tu ywele lakn tra hawajaniacha kwasababu tu ndo kazi nilio izoe ko Mimi kazi Yangu sinufaiki na chochote unawapa waw o tu tra dodoma