🔴Live: YANGA WANATOA TAMKO ZITO BAADA YA MAHAKAMA KUAMURU UONGOZI WA AKINA HERSI UACHIA NGAZI

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 27. 08. 2024
  • 🔴Live: YANGA WANATOA TAMKO ZITO BAADA YA MAHAKAMA KUAMURU UONGOZI WA AKINA HERSI UACHIA NGAZI
    Uongozi wa Yanga unatoa kauli hiyo kufuatia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam, imeamuru Uongozi wa Club ya Yanga ukiongozwa na Rais wa Yanga Injinia Hersi Saidi na wenzake, kuachia ngazi na kuondoka kwenye Club hiyo kwakuwa Katiba ya Yanga haitambui uwepo wao.
    Imedaiwa kuwa uamuzi huu wa Mahakama umekuja baada ya Kundi la Wazee wachache waliowahi kuwa Wazee wa Yanga kipindi cha nyuma, kushitaki Mahakamani likidai uwepo wa Viongozi wa sasa wa Yanga (Injinia Hersi na wenzake) ni batili na haujafuata Katiba ya Club hiyo.
    Kutokana na Wazee hao kushinda kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, inamaana kuwa Rais wa Yanga Injinia Hersi na Viongozi wenzake wanatakiwa kuachia ngazi na kukabidhi Ofisi kuanzia sasa.
    Injinia Hersi alianza kuiongoza Yanga kama Rais miaka miwili iliyopita baada ya kushinda nafasi hiyo akiwa ni Mgombea pekee July 2022 na kumfanya kuwa Rais wa kwanza wa Yanga SC toka kuanza kwa mfumo mpya wa mabadiliko ambapo alitangazwa kuwa atakuwa madarakani kwa miaka minne (hadi 2026) kwa mujibu wa Katiba ya Club hiyo.

Komentáře • 3

  • @amp1952
    @amp1952 Před měsícem

    Nawaza tu kwa sauti, iweje Hakimu wa hiyo kesi asijiridhishe kwanza kama wadai na wadaiwa wana sifa za kusikilizwa. Je, kwa Klabu kubwa kama Young Africans inakosa mawakili wa kuiwakilisha kiasi cha hakimu kutoa hukumu ya upande mmoja! Du😮

  • @NdagiMalida
    @NdagiMalida Před měsícem

    Tuwe makini na wutu wanaotaka kuivuruga yanga na si yanga ni soka la Tanzania

  • @NdagiMalida
    @NdagiMalida Před měsícem

    Muwe kakini muda wote wasaliti hao wapo tuwakabili wasipate nafasi tu😂