Sakata la mgomo wa biashara latua bungeni, Mwigulu afafanua 'migomo inaturudisha nyuma'

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 25. 06. 2024
  • Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba amewataka wafanyabiashara kuacha mgomo wa mara kwa mara, kwani kufanya hivyo inarudisha nyuma juhudi za Serikali kuliletea Taifa maendeleo.
    Amesema hayo leo Jumatano Juni 26, 2024 bungeni jijini Dodoma, alipokuwa akichangia mjadala wa kupitisha Bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/2025 pamoja na kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizotolewa na wabunge wakati wakichangia mjadala yao.
    Mgomo huo wa wafanyabiara ulianza Kariakoo, jijini Dar es Salaam Jumatatu Juni 24, 2024 na mpaka sasa umeshafika katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Mbeya, Iringa, Mtwara na Tunduma Mjini.

Komentáře • 3

  • @barakamanga5502
    @barakamanga5502 Před 4 dny

    Mtuwa mungu kusikiliza siyo kutenda mliyo kubaliana, mwanasiasa anaweza kukusikiliza mwezi akitoka anakupuuzatu, please fikeni mwafaka yasitukute ya kenya, hii ni nchi tulivu, saana,

  • @DensonKaboneka
    @DensonKaboneka Před 4 dny

    Kuongea ni rahisi tu biashala ni pasua kichwa

  • @djtrdtz
    @djtrdtz Před 4 dny

    Hamna cha maana alichoongea utumbo tu