YANAYOJIRI BAADA YA ZIWA TANGANYIKA KUFUNGWA || WAVUVI WARUDISHA MITUMBWI, HALI YAZIDI KUWA MBAYA

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 17. 05. 2024
  • Zikiwa zimepita siku tatu tangu Ziwa Tanganyika lifungwe Mei 15, 2024 dagaa wamepanda bei kufikia Sh70,000 kwa kilo moja huku wafanyabiashara wakilalamika.
    Wafanyabiashara
    Kama ambavyo Serikali ilielekeza shughuli za uvuvi zisimame hadi itakapofika Agosti 15, mwaka huu.
    Wavuvi wametii amri hiyo huku wakihamisha mitumbwi yao katika Mwalo wa Katonga na kuipanga vizuri pembeni huku nyavu wakizifunga, kuzipakia na kuzihamisha.
    Sababu Ziwa kufungwa
    Serikali imefikia hatua hiyo iliyotakiwa kufikiwa tangu mwaka 2023, baada ya makubaliano ya kusimamisha shughuli za uvuvi kwa kipindi hicho yaliyoazimiwa mwaka 2022 na nchi za Zambia, Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zinazozungukwa na ziwa hilo.
    Hata hivyo, ilihairisha uamuzi wake na kuutekeleza mwaka huu.
    Nchi hizo zilikubaliana kwa kanuni moja ya kutambua zana haramu za uvuvi ili kuruhusu mazalia ya samaki kwa wingi na kudhibiti uvuvi haramu, uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi.
    Katika makubaliano baina ya nchi hizo, ziwa hilo litapumzishwa kwa miezi mitatu yaani Mei 15 hadi Agosti 15 kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo ikiwa ni kutoa nafasi kwa samaki kuzaliana.
    Katika kipindi hicho, nchi wanachama wa ziwa hilo watafanya utafiti wa kiwango cha samaki, utafiti wa kibaolojia na matokeo ya kiuchumi kwa watu wanaotegemea ziwa hilo kimaendeleo.
    Insert Naibu Waziri Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti

Komentáře • 3

  • @Hassan-bq8bg
    @Hassan-bq8bg Před 20 dny

    Nchi hii kilasehem nikupiga mungu anawaona hicho mnachokizalisha

  • @Ambeniwatano
    @Ambeniwatano Před měsícem

    Wanatafuta uzuke wizi mitahani hayo mambo ya kufunga ziwa ni uroho mbaya ziwa limeumbwa na mungu samaki wanaumbwa na mungu toka Karne na Karne mababu na mababu mbona awajawai kufunga na samak walikuwepo mungu ni mjuz wa wajuz mwenye uruma kwa watu wake

  • @GibsonNtamamilo
    @GibsonNtamamilo Před měsícem

    Washamba ninyi. Mmevua muda mrefu hamuwekezi kwenye vyanzo vingine mnategemea Uvuvi tu. Kigoma kuna mambo mengi yakufanya na unapata fedha.