Mafuriko Morogoro! Mamia washindwa kusafiri, maji yatanda kila kona

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 4. 05. 2024
  • Mvua kubwa ambayo imenyesha kwa zaidi ya saa 12 wilayani Kilombero mkoani Morogoro imesababisha adha kwa wananchi wa Ifakara baada ya maji kujaa na kusababisha mafuriko, maji yanapita juu ya barabara, na abiria wanavushwa kwa kamba maalumu.
    Mkuu wa wilaya ya Kilombero Dunstan Kyobya akizungumza na Mwananchi Digital leo Mei 5, 2024 amesema tangu ahamie katika wilaya hiyo haya ndiyo mafuriko makubwa zaidi kuwahi kuyashuhudia.
    Kiongozi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kilombero Inspekta Haji Maduluka amesema kinachoendelea ni kuwavusha watu kwa kutumia kamba maalumu ili wasisombwe na maji.
    Wafanya biashara na wasafiri wanaeleza kuwa hali hii ya maeneo yao kujaa maji hawajaishuhudia kwa muda mrefu.

Komentáře • 23