RC MWANZA AWAONYA WAKUU HAWA WA WILAYA/AWAAMBIA MADEREVA WAO WASIKUBALI WAKIWALAZIMISHA

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 7. 07. 2024
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Said Mtanda amekabidhi magari matatu mapya kwa ajili ya Wakuu wa Wilaya za Ilemela, Misungwi na Sengerema, yenye thamani ya Tsh. milioni 684 ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na kuleta maendeleo ya Mkoa huo.
    Akiongea leo katika hafla fupi ya makabidhiano hayo nje ya viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mtanda amesema anamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuruhusu na kuidhinisha fedha kwa ajili ya kuwapatia Wakuu wa Wilaya vitendea kazi.
    "Sisi Wakuu wa Mikoa nguvu yetu kubwa ni Wakuu wa Wilaya na wao wana maeneo yao ya usimamizi, hivyo ukiwa na viongozi hao hodari na wazuri basi kazi yangu pia itakua nyepesi, hivyo ninawapongeza wote kwa uchapaji kazi licha ya kutokuwa na vitendea kazi". Mkuu wa Mkoa.
    Aidha Mtanda ametoa wito kwa madereva wa magari hayo kuhakikisha wanayafanyia ukaguzi kila mara baada ya kutembea kilomita elfu 50 na wawapatie taarifa viongozi wao mara baada kufikisha kilometa hizo ili wawaruhusu wakafanye ukaguzi wa magari (Service) hali ambayo itapelekea kuviimarisha vyombo hivyo.
    "Na nyie madereva hata kama Mkuu wako wa kazi atasema tusafiri tu mwambie hapana tufanye service ya gari kwanza , na nyie viongozi wasikilizieni madereva wenu, wakiwaambia gari haiwezi kusafiri msiwalazimishe maana hao ndio wataalamu wa vyombo hivyo". Amesisitiza Mtanda wakati wa makabidhiano hayo
    "Msipofanya hivyo mtaisababishia hasara Serikali kwani imetumia na kuwekeza fedha nyingi katika kuwaleteeni ninyi vitendea kazi hivi na nchi hii ina wakuu wa Wilaya wengi ambao bado wana uhitaji wa magari". Mhe.Mtanda
    Kadhalika Mkuu huyo wa Mkoa amesema ikiwa tunaelekea katika harakati za uchaguzi, shughuli zitakua ni nyingi kwa Wakuu wa Wilaya zikiwemo za ufuatiliaji, usimamizi, na ukaguzi hivyo amesema atajielekeza pia katika kuhakikiaha Wakuu wa Wilaya za Magu na Ukerewe na wao wanapatiwa vitendea kazi ili kurahisisha utimizaji wa majukumu yao.
    Akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya waliokabidhiwa vitendea kazi hivyo, Mhe. Johari Samizi Mkuu wa Wilaya ya Misungwi amesema kwa takribani miaka 3 amekua akitumia gari tofauti za Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi hivyo kupokea gari hiyo mpya itapelekea sasa gari zile alizokua akitumia zikatumike katika shughuli nyingine.

Komentáře • 2