Rais Magufuli ‘amkaanga’ hadharani Mkurungenzi Butiama kisa mamilioni ya ujenzi wa hospitali

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 5. 09. 2018
  • Rais Magufuli amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama mkoani Mara Mabula Alphonce kushughulikia haraka ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo, huku akibainisha kuwa tayari kuna fedha kiasi cha shilingi milioni 400 ambazo tayari zimetolewa.
    Rais Magufuli amemuita mkurugenzi huyo mbele ya wananchi na kumtaka kuzitumia fedha hizo kwanza kabla ya kuomba fedha nyingine, huku akiahidi kumfuatilia.
    Ni katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Septemba 6 kwenye Uwanja wa Mwenge wilayani Butiama, mkoani Mara.

Komentáře • 141