KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA MORNING GLORY : THE SCHOOL OF HEALING 31/ 07/ 2024

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 7. 09. 2024
  • KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA MORNING GLORY : THE SCHOOL OF HEALING 31/ 07/ 2024
    SEMINA YA NENO LA MUNGU: SADAKA, UKUHANI NA MADHABAHU
    UJUMBE WA LEO: NGUVU YA MADHABAHU YOYOTE INATEGEMEA AINA YA IBADA NA SADAKA ZINAZOTOLEWA JUU YAKE
    MAANDIKO:
    Kutoka 23 : 32
    1 Wafalme 11 : 5 - 7
    2 Wafalme 23 : 10 - 13
    2 Wafalme 3 : 26 - 27
    Waamuzi 10 : 6
    Waamuzi 11 : 30 - 31
    32 Usifanye maagano pamoja nao, wala pamoja na miungu yao.
    Hii ni madhabahu ya mungu Moleki, mungu wa Waamoni ambaye Sadaka iliyokuwa ikihitajika juu ya madhabahu ili kuiwezeshasha kuwa na nguvu ilihitajika SADAKA ya watoto wachanga ili kulitengeneza agano, au kuliimarisha agano

    1 Wafalme 11 : 5 - 7
    5 Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni.
    6 Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.
    7 Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la Wamoabi,
    mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni.
    2 Wafalme 23 : 10 - 13
    10 Naye akainajisi Tofethi, iliyomo katika bonde la wana wa Hinomu, ili mtu asipitishe mwana wake au binti yake motoni kwa Moleki.
    11 Akawaondoa farasi ambao wafalme wa Yuda waliwatoa kwa jua, hapo pa kuingia nyumbani mwa Bwana, karibu na chumba cha Nathan-Meleki, towashi, kilichohuwako kiungani; akayapiga moto magari ya jua.
    12 Nazo madhabahu zilizokuwako darini juu ya chumba cha juu cha Ahazi, wafalme wa Yuda walizozifanya, nazo madhabahu alizozifanya Manase katika behewa mbili za nyumba ya Bwana, mfalme akazivunja, akazitelemsha huko nje, na kuyatupa mavumbi yake katika kijito cha Kidroni.
    13 Na mahali pa juu palipokuwapo mbele ya Yerusalemu, palipokuwa upande wa kuume wa mlima wa uharibifu, alipopajenga Sulemani, mfalme wa Israeli, kwa Ashtorethi, chukizo la Wasidoni, na Kemoshi, chukizo la Moabu, na Milkomu, chukizo la wana wa Amoni, mfalme akapanajisi.
    Hii ni madhabahu ya miungu ya Wamoabi ambaye sadaka yake kuu ilikuwa watoto kulingana na hitaji la madhabahu

    2 Wafalme 3 : 26 - 27
    26 Naye mfalme wa Moabu alipoona ya kwamba ameshindwa vitani, alitwaa pamoja naye watu mia saba wenye kufuta panga ili wapenye hata kwa mfalme wa Edomu; wala hawakudiriki.
    27 Ndipo akamtwaa mwanawe wa kwanza, yeye ambaye angetawala mahali pake, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa juu ya ukuta. Kukawa hasira kuu juu ya Israeli; basi wakatoka kwake, wakarudi kwenda nchi yao wenyewe.
    Waamuzi 10 : 6
    6 Kisha wana wa Israeli walifanya tena yaliyo maovu mbele za macho ya Bwana, wakawatumikia Mabaali, na Maashtorethi, na miungu ya Shamu, na miungu ya Sidoni, na miungu ya Moabu, na miungu ya wana wa Amoni, na miungu ya Wafilisti; nao wakamwacha Bwana, wala hawakumtumikia yeye.
    Waamuzi 11 : 30 - 31
    30 Naye Yeftha akamwekea Bwana nadhiri, akasema, Kwamba wewe utawatia wana wa Amoni mkononi mwangu kweli,
    31 ndipo itakuwa ya kwamba, kile kitakachotoka katika milango ya nyumba yangu kunilaki, hapo nitakaporudi na amani kutoka kwa hao wana wa Amoni, kitu hicho kitakuwa ni cha Bwana, nami nitakisongeza kiwe sadaka ya kuteketezwa.
    Hii ni miungu ya Kanaani na Foinike iliyojulikana sana kama watawala wa hali ya hewa,kuongeza ustawi wa ardhi na uzao wa wanyama na wanadamu. Madhabahu iliinuliwa juu vilele vya milima walivyoviweka wakfu na kupaita Mahali pa juu"palipopatikana BAALI kwa mwonekano wa mwanamume na ASHTORETHI katika mwonekano wa Mwanamke.

    Mhubiri: Mwl. Elirehema Palangyo.
    Kwa maombi na ushauri :
    Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
    Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
    Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
    Simu: +255 713 553 443
    CZcams: Kijitonyama Lutheran church
    Barua Pepe: Kijitonyamalutheran@gmail.com

Komentáře • 21