WAZIRI MKENDA AKANUSHA WENYE GPA CHINI YA 3.8 KUONDOLEWA SIFA ZA KUPATA KAZI

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 17. 08. 2023
  • Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amekanusha taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na watu wasio na nia njema kuhusu wanafunzi ambao hawatafikia ufaulu wa GPA ya 3.8 wataondolewa sifa za kupata ajira.
    Waziri Mkenda amewasihi wananchi kupuuza taarifa hizo na kusema kuwa Wizara yake haihusiki na ajira na kuwa taarifa hizo ni za uongo.
    Prof. Mkenda pia ametoa ufafanuzi kuhusu utaratibu w ufadhili wa Samia Scholarship ambapo amesema wanafunzi hao wasipogikisha GPA 3.8 wataondolewa katika ufadhili huo na kuwekwa kwenye mikopo lengo likiwa kuwataka wanafunzi hao kuendelea kusoma kwa bidii
    Amesema kuwa wanafunzi hao wamesaini mkataba na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambao pamoja na mambo mengine unawataka kuhakikisha wana endelea kupata matokeo mazuri na kusomea masomo ya sayansi, Hisabati, Uandisi na Elimu tiba na hawaruhusiwi kubadilisha.
    Follow us on:
    FACEBOOK;
    SpotiLeo: / spotileo-176. .
    HabariLeo: / habarileo
    DailyNews: / dailynewstz
    INSTAGRAM;
    HabariLeo: habarileo_tz?ig...
    SpotiLeo: spotileo?igshid...
    TWITTER;
    Twitter HabariLeo: HabariLeo?s=09
  • Zábava

Komentáře • 1

  • @severinkinunda5269
    @severinkinunda5269 Před 4 měsíci

    Tukiangalie tu habari za GPA tuangalie ubunifu. Kuna watanzania wengi wana GPA first class lakini wapo hawana ajira wameshindwa hata kujiajiri. Elimu bora sio kuwa na GPA tu bali chachu cha kuleta mabadiriko ktk jamii