KUELEKEA MNADA WA KWANZA WA CHAI KUFANYIKA NCHINI TANZANIA

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 9. 11. 2023
  • Mwandishi Wetu
    KATIKA kuhakikisha zao la chai linachangia kukuza pato la taifa, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeanzisha mnada wa chai utakaokuwa ukifanyika hapa nchini kwa lengo la kuongeza thamani ya zao hilo.
    Mnada wa kwanza wa chai utafanyika Jumatatu- Novemba 13, mwaka huu kwenye jengo la Millenium Tower, Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Bodi ya Chai Tanzania.
    Kwa miaka mingi Tanzania imekuwa ikitumia mnada wa chai wa Mombasa nchini Kenya hatua ambayo imekuwa ikikumbana na changamoto kadhaa ikiwemo ya umbali wa kutoka kwenye mashamba ya chai hapa nchini hadi kufikia kwenye mnada huo nchini Kenya.
    Akizungumzia hatua ya kuanza kwa kufanyika kwa mnada wa chai hapa nchini, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai, Mary Kipeja anasema itapunguza gharama za kimasoko za wasindikaji, mfano gharama ya kusafirisha chai hadi Mombasa-Kenya itapungua kwa asilima 50 hali itakayoleta unafuu kwa wakulima.
    Naye mkurugenzi mkuu wa wakala wa maendeleo ya washika dau wadogo wa chai nchini, Theophord Ndunguru amesema hii nifursa kwa wakulima wa chai na vyama vya ushirika wa chia nchini kwenye kujiendeleza kiuchumi kwani mihatua hii ya bodi ya chai kuzindua minada ya chai nchini kutakuza sekta ya kwa kuongeza kipato kwa wakulima hivyo kuwasisitiza kwenye uwekezaji wa viwanda vidogo vidogo vya kusindika chai kwenye maeneo yao.

Komentáře • 2

  • @MpangoMzima
    @MpangoMzima Před 5 měsíci

    Me nahitaji na niko zanzibar

  • @MpangoMzima
    @MpangoMzima Před 5 měsíci

    Haya maghala yana patikana wap