MAKAMU WA RAIS ACHUKIA/UJENZI WA BARABARA HII KIGOMA WAMKERA VIBAYA/AMPA MAAGIZO WAZIRI BASHUNGWA

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 8. 07. 2024
  • Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa kuhakikisha anasimamia ujenzi wa barabara ya Malagarasi - Ilunde - Uvinza (km 51.1) kwa kiwango cha lami ukamilike ifikapo mwezi Machi, 2025.
    Dkt. Mpango ametoa agizo hilo leo Julai 8, 2024 katika eneo la Malagarasi wakati akikagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Malagarasi - Ilunde - Uvinza kwa kiwango cha lami na kuridhishwa na maendeleo yake.
    “Hii barabara imesuasua sana hasa kipindi cha mvua, na huku Kigoma bado tunapata mvua nyingi kwa hiyo Waziri tutumie kipindi hiki cha kiangazi kukimbiza hii barabara iishe kama ulivyoahidi na sisi tupite hapa tukiwa tumevaa suti, Simamieni hili Waziri pamoja timu yako”, ameeleza Dkt. Mpango.
    “Ni maelekezo yako Mheshimiwa Makamu wa Rais, umechoka na ule usemi wa Kigoma mwisho wa reli, badala yake Kigoma iwe mwanzo wa reli na sisi Wizara ya Ujenzi tunaenda kutekeleza hilo kuhakikisha mkoa huu unakuwa Mwanzo wa reli katika sekta ya Miundombinu”, amesisitiza Bashungwa
    Aidha. Bashungwa ameeleza kuwa Wizara ya Ujenzi imekamilisha kufanya usanifu wa barabara kuanzia Kibaoni kuelekea Kasulu na hatua iliyopo hivi sasa ni kuendelea kufanya mazungumzo na mfadhili ili nayo iweze kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami.
    “Mheshimiwa Makamu wa Rais nikuahidi Wizara ya Ujenzi hatutakuwa kikwazo kwa dhamira yako ya kusaidia Mkoa wa Kigoma kupata maendeleo, kwahiyo barabara hii ya kibaoni kwenda Kasulu tunaendelea na mazungumzo ili tutakapokamilisha ujenzi wa kilometa 51.1 ya barabara ya Malagarasi - Uvinza basi na kipande cha Kibaoni - Kasulu kianze kujengwa kwa kiwango cha lami”, amefafanua Bashungwa.

Komentáře • 2

  • @brunomirambi8792
    @brunomirambi8792 Před 16 dny

    UBORA WA HIYO BARABARA MH: UMEPITA KWA BAADHI YA VIPANDE VYAKE?? GARI HALINA UTULIVU UTAFIKIRI BADO UKO KWENYE BARABARA YA VUMBI MIMI BINAFSI HIYO NI KODI YETU BARABARA HIYO HAIFAI UBORA HAMNA KABISAAA