FULL VIDEO: Ruge Mutahaba Afunguka Kuhusu RC Paul Makonda Kuvamia Ofisi za Clouds

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 19. 03. 2017
  • Ruge Mutahaba anafunguka jinsi Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alivyovamia ofisi za Clouds Media wakati kipindi cha Shilawadu kikiwa hewani.
    Mtandao wa Global Publishers, www.globalpublishers.co.tz umeiandika habari hii kwa kina ambapo inaelezwa kwamba
    Meneja wa kampuni ya Clouds Media Group (CMG) Ruge Mutahaba siku ya jumatatu Machi 20 aliamkia katika kipindi cha Clouds 360 kuzungumzia issue ya RC Paul Makonda kuvamia ofisi za Clouds na askari wenye bunduki kwa madai ya kuwa Clouds TV waligoma kurusha kipande cha kipindi cha SHILAWADU kilichokuwa kina muonyesha mdada anayesemekana kuwa amezaa na Mchungaji Gwajima.
    RC Paul Makonda aliibuka kwenye ofsi za kampuni hiyo mida ya usiku akiwa na askari wake na kuingia moja ka moja ndani ya studio za Clouds kuuliza kwanini kipande hicho kilikatishwa.
    Taarifa za uvamizi wa RC Paul Makonda zilimfikia Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joeseph Kusaga na General Manager wa kampuni hiyo Ruge Mutahaba ambao baada ya kupokea taarifa hizo waliwasiliana na RC Paul Makonda na kujaribu kufafanua utaratibu wa kwa nini kipindi hiko kilisitishwa.
    Akizungumza LIVE siku ya jumatatu kupitia kipindi cha Clouds 360 Ruge Mutahaba alifunguka na kusema:
    "Mkuu wa Mkoa Paul Makonda alinipigia na kuuliza kwa nini kipindi chake kimekatisha... nikamuuliza kipindi gani? Akasema kuna kipindi kilikuwa kinaruka hapa lakini kimesitishwa, nikamwambia hapana Mkuu mimi kama Mkurugenzi wa vipindi ninauwezo wa kusema kipindihiki kiruke ama kisiruke., akanijibu sawa na kisha akakata simu"
    Kilichoendelea baada ya hapo hakikujulikana ila kwa mujibub wa Ruge Mutahaba, RC Paul Makonda aliamua kuchukua flash iliyokuwa na video hiyo ya kipindi cha SHILAWADU na kuondoka nayo.
    " Sijui nini kilichoendelea baada ya hapo maana sikuenda ofisini mara moja ilanilivyofika niliambiwa Mkuu wa Mkoa amechukua flash iliyokuwa imebeba kipindi hicho ambacho kilikuwa ni kipindi cha SHILAWADU..."
    Ruge Mutahaba aliedelea kufunguka na kusema kuwa kitendo alichokifanya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda cha kuvamia ofisi za Clouds Media Group usiku akiwa na askari wenye bunduki hakikuwa sahihi kwani kama kulikuwa na tatizo ama jambo kuna utaratibu wa namna ambavyo wanapaswa kuwajibiwa akiendeleakusema kuwa alichokifanya ni kuikosea kampuni yake heshima na kuwajaza hofu wafanyakazi wake wa Clouds ( akina SHILAWADU) ambao walikuwa wanafanya tu kazi yao.
    Aliongezea kusema kuwa urafiki alionao na RC Paul Makonda ulianza mbali kabla hata ya yeye kuwa Mkuu wa Mkoa hivyo angependa kuendelea kushirikana naye pamoja na Serikali ya Awamu ya tano ila atambue tu alichokifanya hakikuwa sahihi na kwa njia moja ama nyingine amewakosea sana heshima.
    Msikilize Ruge Mutahaba Akifunguka Kuhusu RC Paul Makonda Kuvamia Ofisi Za Clouds hapo juu.
    Kaa karibu nasi kupitia mitandao ya kijamii:
    Instagram: / globalpubli. .
    Twitter: / globalhabari
    Facebook: / globalpublis. .
    Tembelea website yetu kwa habari za kila siku: www.globalpublishers.co.tz
    Unaweza kusubscribe youtube channel yetu kwa kubofya
    / uwazi1
    / uwazi1
    / uwazi1

Komentáře • 4

  • @lukasnkane2919
    @lukasnkane2919 Před 7 lety +1

    Walimlea, anawageuka.

  • @nyanda427
    @nyanda427 Před 7 lety +1

    Issue nzima ipo ambiguous; we need to hear from someone ambae alikuwa pale wakati RC anaingia, pili tunataka details kutoka kwa watu aliorecord kipindi, tatu huyo mama walimpata wapi? nne Gwajima alijuwa vipi kama studio kuna kipindi chake? nachokiona hapa studio kuna team Gwajima na team Makonda. Isitoshe nani kaziachia clips za CCTV zikimuonesha RC wakati akiingia na Mmeziachia ili iweje na kwa maelekezo ya nini?. Maelezo yako yote yana validate msimamo wenu juu ya Makonda vs Gwajima. Nasema haya kwa sababu ya headline mnayoitumia (mmevamiwa) wakati hata backup ya hoja yenu ipo shallow. Pili kitendo cha kuachia hiyo clip katika social network. Tatu, mnavyo address tukio Zima mnaonekana mmenunuliwa na upande wa pili

  • @EcoEssence_wellness
    @EcoEssence_wellness Před 7 lety

    Ni shida...

    • @godelivamuhumuza8304
      @godelivamuhumuza8304 Před 7 lety +1

      Kabla ya madawa ya kulevya haya yote yalikuwa hayatokea hayoyanayotokea sasa hasa kwa huyu kijana uktukanwa kwenye Ibada na waumini wanashangilia kama ni kumtukuza Mungu.Watu kama hawana akili nzuri na hakuna wa kuchukua hatua.