YANGA SC 2-2 BIASHARA UNITED: MAGOLI NA MIKWAJU YA PENATI (5-4): (ASFC - 31/01/2019

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 30. 01. 2019
  • Vijana wa Jangwani, Yanga SC leo wamefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) baada ya kuitupa nje Biashara United kwa mikwaju ya penati 5-4 kufuatia sare ya mabao 2-2 katika muda wa kawaida wa dakika 90.
    Mchezo huo wa raundi ya nne ya michuano hiyo umepigwa kwenye Dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam na kushuhudia wenye Yanga wakifanya kazi ya kusawazisha kila wanapofungwa.
    Biashara United walianza kwa bao la penati lililofungwa na Wazir Jr. dakika ya 3 kabla ya Yanga kusawazisha kupitia kwa Amissi Tambwe akifunga kwa penati pia dakika ya 9.
    Biashara United wakaongeza bao kupitia kwa Innocent Edwin dakika ya 40, lakini Yanga wakaongeza kasi ya mashambulizi na kufanikiwa kuchomoa bao hilo dakika ya 74 kupitia kwa Heritier Makambo na kufanya mchezo umalizike kwa sare y mabao 2-2.
    Ilipofuata mikwaju ya penati, Yanga walifunga penati zote tano kupitia kwa Heritier Makambo, Paul Godfrey, Ibrahim Ajibu, Thabani Kamusoko na Matheo Anthony, huku Biashara United wakikosa penati moja iliyopigwa na Tariq Seif.
  • Sport

Komentáře • 251