Fursa za kiuchumi tunazo lakini watu wetu hawaidiki nazo, tunahitaji mageuzi-OMO

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 21. 06. 2024
  • Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman, leo Ijumaa Juni 21, 2024 amejumuika na Waumini wa Kiislamu, katika Ibada ya Sala ya Ijumaa, hapo Msikiti wa Ijumaa Kigunda, uliopo Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
    Baada ya Sala hiyo, Mheshimiwa Alhaj Othman ametoa salamu zake mbele ya Waumini akisema, ni busara kuendelea kushikamana na Mafunzo Mema ya Dini, yakiwemo malezi bora ya watoto na kuwalea katika Imani sahihi; huku akihimiza umuhimu wa jamii kujenga moyo wa kusameheana kwa dhati.
    Akitoa Khutba Mbili za Ibada hiyo ,Sheikh Vuai Ame wa Nungwi, amehimiza umuhimu wa waumini wa Kiislamu kutoa Sadaka ili kupata Msamaha na kukutana na Mwenyezi Mungu Akiwa Anewaridhia.
    Mara baada ya Ibada hiyo Alhaj Othman, alitembelea Maeneo ya Vivutio vya Utalii vya 'Mnarani Aquarium' Baraka 'Natural Aquarium' na Mnarani 'Beach Cottages', vyote vya hapo hapo Nungwi.
    Viongozi mbali mbali wa Serikali na Vyama vya Siasa wameambatana na Alhaj Othman katika Ibada hiyo, wakiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini 'A' Unguja, Bw. Othman Ali Maulid ; na Mstahiki Meya wa Kaskazini 'A' Unguja, Bw. Machano Fadhil Machano.
    Kitengo cha Habari,
    Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,
    Juni 21, 2024.

Komentáře • 1