HILA ZIMEVUNJWA Na Bernard Mukasa - QUADRI V

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 6. 09. 2024
  • HILA ZIMEVUNJA
    Mtunzi:
    BERNARD MUKASA
    Waimbaji:
    QUADRI V (Familia ya Bernard Mukasa na Matilder Sendwa Mukasa na watoto wao)
    Kinanda:
    VINNY MUKASA
    Audio & Video:
    HOLY TRINITY STUDIOS
    (Studio ya Utatu Mtakatifu)
    MANENO YA WIMBO
    1. Mungu alipopanga ukombozi, kusudi kutuosha dhambi hizi;
    Akakubali kwamba ye'mwenyezi, afe kifo kibaya kionezi.
    Mti wakamuwamba kama mwizi, wakidhani ya kwamba ameshindwa.
    Kiitikio:
    Amefufuka Bwana na mwokozi, kazivunja hila za Lusiferi.
    Katukomboa wana wa mwenyezi, twaimba ndiyo maana nyimbo nzuri.
    2. Mungu akakubali kuonewa, hakuweka wakili kutetewa.
    Nguo bila hiari kavuliwa, kapigwa misumari kazomewa.
    Akabaki kusali kuombea, wauaji wapate msamaha.
    3. Mungu atufundisha kujitoa, ya wengi maisha kuokoa.
    Na anatukumbusha kupokea, yanayotutisha kumwendea.
    Tusije kukatisha njema nia, ili kuyapisha ya dunia.
    ENGLISH TRANSLATION
    (Translated by Rev. Fr. Renatus Mashishanga)
    1. When God planned salvation, in order to cleanse our sins;
    He accepted, the Almighty to die an unpleasant death, an absurd death.
    They nailed him on a tree like a thief, thinking that he has failed.
    Chorus:
    He has risen, lord and saviour, He has broken Lucifer's tricks.
    He has saved us children of the Almighty; We are singing, this is the meaning of the sweet songs.
    2. God accepted being oppressed, he didn't put an advocate to plead for him.
    His garments stripped off without his will, they sailed him, booed him.
    He remained praying interceding, murderers may be forgiven.
    3. God teaches us to sacrifice ourselves to save others lives.
    And he reminds us to accept whatever terrifies us to approach him.
    So that we may not end the good intention in order to Passover the worldly things.

Komentáře • 244