Ziara ya Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Salum Haji Othman kwa Walinda Amani Afrika ya Kati

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 3. 09. 2022
  • ZIARA YA MNADHIMU MKUU WA JWTZ NCHINI CAR
    Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salum Haji Othman amefanya ziara maalum katika Kikosi cha walinda amani kutoka Tanzania kinachohudumu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
    Luteni Jenerali Salum Othman akiwa na ujumbe wake wamewasili katika uwanja wa ndege wa Berberati uliopo katika Mkoa wa Mambere Kadei na kupokelewa na Mwenyeji wake Kamanda Kikosi TANBAT 05 Luteni Kanali Adam Hamis Kiza, Maafisa na Askari mbalimbali wanaohudumu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa, MINUSCA hapa Jamhuri ya Afrika ya kati.
    Luteni Jenerali Othman amepokelewa na gwaride la heshima lililoandaliwa na TANZBAT 5 na baadae kupokea taarifa ya utendaji kazi ya Kikosi Kutoka kwa Afisa Mkuu wa Operesheni Meja Amulike Kabale.
    Pamoja na mambo mengine Luteni Jenerali Salum Othman amepata wasaa wa kufanya mazungumzo na Kamanda Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi wa Amani - MINUSCA Luteni Jenerali Sidiki Traole yanayolenga utendaji kazi wa Kikundi cha walinda amani wa Tanzania.
    Aidha, alipata fursa ya kufanya mazungumzo na maafisa na askari katika ukumbi wa Serengeti ambapo walinda amani hao walionesha ari, hamasa na utayari wa kutekeleza majukumu ya ulinzi wa amani huku wakifata sheria na taratibu za Umoja wa Mataifa, pamoja na za nchi husika.
    Katika ziara hiyo Luteni Jenerali Salum Othman ameambatana na Mwambata Jeshi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa nchini marekani Brigedia Generali George Mwita Itang’are, Kanali Ally Juma Ally, Kanali AbdulAziz Rashid, Kanali Mustapha Mussa Hozza, Luteni Kanali Jofrey Clemence Kilyenyi, Meja Mariam Godian Tabaro na Kapteni Hemed Athumani Mwalim.

Komentáře • 1

  • @AnwarOmari-qx9qz
    @AnwarOmari-qx9qz Před 3 dny

    Hongereni jeshi letu hakika muna jitoa sana kuiletea nnchi yetu heshima