JINSI YA KUSHINDA HILA ZA SHETANI - PASTOR SUNBELLA KYANDO

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 21. 09. 2021
  • "Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;"
    1 Petro 2:9
    Sisi sote tuliompokea Yesu Kristo katika ulimwengu wa roho tunaonekanika kama makuhani.
    Na kama wewe ni kuhani na hauna maarifa Mungu atakukataa, kwanini? Kwasababu maarifa ndiyo yanakuwezesha kuifanya kazi yake kwa urahisi na kwa ubora.
    Maarifa unapewa na Mungu au unayapata kwa kusikiliza neno la Mungu.
    Mungu anataka makuhani tuwe na maarifa kwasababu adui yetu anafanya kazi kwa hila(ujanja ujanja)
    "Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
    Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza KUZIPINGA HILA za Shetani."
    Waefeso 6:10-11
    Tunachoshindana nacho kwa adui sio nguvu zake, ni hila zake, HILA ni "kupretend" una kitu fulani wakati HAUNA.
    Kitu ambacho adui anafanya ni kumtoa mtu kwenye "comfort zone" na akishamtoa kila kitu chake huyo mtu kinaharibika. Kitu Mungu huwa anafanya ni kumtumia kuhani kumrudisha huyo mtu kwenye comfort zone yake.
    Kuna vitu vingi unapambana navyo kwenye maisha ni kwasababu hauna maarifa, haujatumia nguvu kubwa kuongeza maarifa ya kukusaidia. Sisi "The reality Of Christ church" asilimia kubwa ya mafundisho yetu ni namna ya kudeal na adui, namna ya kuona tatizo kwa jicho jingine, namna ya kugundua hila za shetani.
    #PastorSubella#Hila#ZaShetani

Komentáře • 12