"Niliacha Kazi Ili Kujitegemea, Nilifilisika, Haikuwa Rahisi" |SALAMA NA DANIEL KIJO PART 1

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 11. 09. 2024
  • #SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
    Kwenye maisha kuna watu ambao ukitutana nao tu unaamini wana kitu kizuri ndani yao na bila ya shaka watakua na mafanikio mengi tu huko mbele tuendako, hii ndo hisia ambayo mimi nimekua nayo toka siku ya kwanza naonana na Daniel Kijo. Mwerevu, mcheshi, ana muonekano mzuri na mkarimu, ila kubwa kabisa ana akili, mgunduzi na mtafutaji hasa, toka siku ya kwanza.
    Ukiachana na kwamba pengine ametoka kwenye familia ambayo kipato chake si kibaya na amesoma shule nzuri sana, Daniel hakuwahi kijikweza na kujiona yeye BORA zaidi ya wengine alionao chumba kimoja.
    Nilikutana nae EATV wakati yeye akiwa bado mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam lakini wakati huo huo anafanya kazi ili mambo yake mengine yaende vizuri. Na kazi alikua anaifanya kwelikweli, ikiwa ya kutaarisha yani kwenda kuitafuta habari na kuifanyia uchunguzi na kuhakikisha inarekodiwa vizuri, na kama itahitaji sauti basi ataiwekea na mwisho kabisa yeye ndo atakua mtangazaji wa hiko kipindi wakati watazamaji wanakiona kwa mara ya kwanza.
    Nadhani utashi huo ndo ulimfanya aone unajua nini, mbona mi naweza kufanya mwenyewe hii? Mbona nisitoke tu hapa na kuanzisha kitu changu mwenyewe? Na hilo alilifanya.
    Daniel ananielezea mitihani aliyopitia baada ya kuamini kama anaweza kufanya shughuli za uzalishaji wa vipindi na mauzo mara baada ya kujikusanyia PENSHENI yake, anakumbuka kama wakati huo ulikua ukiacha kufanya kazi, ulikua na uwezo wa kwenda kuchukua NSSF yako na ukajianzishia biashara yako. Daniel anasema alienda akanunua ma camera na vifaa vyengine akiamini kabisa kama maisha ndo yameanza sasa, ila dunia ndo ilimuonyesha kwamba ki ukweli vitu si RAHISI kama ambayo alikua anadhania. Na kwenye kipindi hiki ndo ambacho aliwajua Ndugu zake ni nani na marafiki zake ni nani. Maana Rhumba lilikua si la NCHI hii.
    Daniel ameshawahi kuanzisha na kufanya vipindi mbali mbali vya TV hapa nyumbani na kwenye TV stations tofauti tofauti kwahiyo ashakutana na mabosi na wafanyakazi wa aina tofauti tofauti sana. Na akiwa huko kwenye safari yake hiyo ndo imemjenga awe huyu ambaye tunampenda na kujifunza kutoka kwake sasa.
    Miaka ya hivi karibuni Daniel amekua akiyafanyia kazi mashirika mbalimbali ya habari ya kimataifa hapa nyumbani na hii ni kazi ambayo yeye na MKE wake walipambana nayo sana mpaka ikadondokea kwenye mapaja yao.
    Daniel pia anatuhadithia jinsi ambavyo alikutana na mke wake, mazingira ambayo walikutana na jinsi ambavyo walianza kuongea, mara ya kwanza alivyompeleka kwa wazazi wake na jinsi ambavyo wanaishi kwa misingi ya kujijali wao na afya zao. Daniel anatuambia jinsi ambavyo anapenda anavyokua anaenda shuleni kwa mtoto wake na kuwa yeye ndo Baba cool kuliko wazazi wengine, na hii anaipambania sana kwasababu ni moja ya vitu vinavyompa raha. Daniel anapenda mazoezi, analinda afya ya akili yake na mwili wake na ni mtu ambaye anajifunza sana, tena kila siku.
    Yangu matumaini episode hii yangu na Rafiki yangu itakusaidia hapa na pale kuhusu kujiamini na kujijali ki mwili na ki roho maana mwisho wa siku, hakuna anayekuja kukusaidia kwenye hayo. Mwisho wa siku hayo ni maisha yako na jinsi gani unataka kuyaishi ki ukweli ni juu yako.
    Tafadhali enjoy,
    Love,
    Salama.
    Support us through anchor.fm/yahs...
    SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahSton...
    Listen our Podcast on
    Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
    ‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
    GooglePodcast Link bit.ly/GoogleP...
    Audiomack Link bit.ly/YahSton...
    ‪CZcams Link bit.ly/CZcamsS...
    Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
    Follow:
    Twitter: / yahstonetown
    Instagram: / yahstonetown
    Facebook: / yahstonetown
    Channel Administered by Slide Digital
    Instagram: slidedigitaltz

Komentáře • 34

  • @mbwanamtessa8607
    @mbwanamtessa8607 Před 2 lety +28

    Daniel kijo, a.ka baba festo mwanao wa kwanza mimi ndiyo nilikuwa dereva wa kumpeleka mkeo clinic muhimbili mpaka kujifungua. Nakumbuka ulikuwa na furaha sana. Na ukanihusia kitu kimoja ukaniambia mdogo wangu ukikuwa utayaona nawewe. Tuko mateniti Ward pale usiku tunamsikilizia mama mtu atoke.

  • @iammichaellukindo
    @iammichaellukindo Před 2 lety +13

    Sijui kwann comments ni chache. Lakini nimekua nikikuona Daniel. Nilikua napata questions sana who are you and what you are. Nilikua nakuona nakua nahs kama unafanikiwa kwa kasi sana. Karibu 80% ya mambo unayo zungumza ni mimi completely. Mm nili quit media kwa woga wa kukwama in the future tena baada tu ya kupata mtoto. Niliogopa sana kuona na turn 30 sina nyumba, sina gari, sina hata kiduka cha mangi Nategemea mshahara tu na hautoshi. Nilitamani sana kuweza kuwa na kitu cha ziada cha kusapoti uchumi wangu ili niinuke kufikia malengo angalao nikiwa na age ya 30. Mambo niliyo weza kufanya 5 years after quiting media job, ni 10 times kuliko NILIPOKUWA nimeajiriwa. So this is so exciting to watch you explaining all this. Thought I was complicated enough to make others mis understand me, but now I know I am not alone.

  • @bekarpaul
    @bekarpaul Před rokem +2

    Japo sisi wengine tumechelewa ktk kufanikiwa lakini hizi Interview huwa zinatufanya tuone kwamba kumbe bado tuna muda wa kutafuta na kufanikiwa... Thanks bro umekuwa icon mnzuri kiukweli.

  • @saumusalimuhassan2499
    @saumusalimuhassan2499 Před 2 lety +1

    Namsikia sana tu uyu Jamaa, ila niko hapa kumjua zaidi, maana toka nimeanza kusikiliza interview ni madini matupu yako hapa,respect *Daniel kijo*

  • @nsajigwamwanjati5119
    @nsajigwamwanjati5119 Před 2 lety +6

    Dan I miss u bro,salama nakupenda sana

  • @TemuTV
    @TemuTV Před 2 lety +3

    KUBWA SANA INTERVIEW IMESHIBA 🙌🙌🙌🇹🇿

  • @kismatiproperty
    @kismatiproperty Před 2 lety +2

    This guy is Genius

  • @titogodwin5701
    @titogodwin5701 Před 2 lety +7

    Boys boys Tv 1 lilikua pindi kali sana

  • @Nature_adventure
    @Nature_adventure Před rokem +1

    We keep learning here.

  • @kazkaz1943
    @kazkaz1943 Před 2 lety +3

    Danny kama danny nakumbuka enz yupo na calor ndos eatv🥰🥰🥰🥰

  • @samsonsitta6127
    @samsonsitta6127 Před 2 lety

    This is one of those DOPE editions. It's a lot of learning. Great job Salama

  • @ModernFlicks
    @ModernFlicks Před 2 lety +3

    Kuna madini mengi sana kwenye hii interview.

  • @tumlakimwaitumule
    @tumlakimwaitumule Před rokem +1

    Well done Salma,kijo salute bro

  • @mkaapwekekariakoo6417
    @mkaapwekekariakoo6417 Před 2 lety +1

    asante sana... Hakika kupata mtoto sio Acceident... THAT'S A PUNCHLINE EVER... Bravo

  • @joesimba
    @joesimba Před rokem +1

    Very nice interview, salama inabidi ajifunze kidogo kuwa ok kupewa compliments, otherwise it was a great show.

  • @mokijr1099
    @mokijr1099 Před 2 lety +1

    Very smart interviewee

  • @sharifsajan7945
    @sharifsajan7945 Před 2 lety +1

    Dan Kijo, kitambo brother, since Mtwara nyakati flani!good to see you

  • @mgayan1222
    @mgayan1222 Před 2 lety

    The new version of the late Mchungaji Daniel Manase Kijo

  • @yusuphaman9294
    @yusuphaman9294 Před rokem +1

    Very interesting interview, well done salama!! Kijo he's smart 🧠

  • @richardcastromzena5136

    Brother from another mother Daniel kijo
    15:18
    20:13 Steal like an artist (book)
    22:46

  • @bluejayz1428
    @bluejayz1428 Před 2 lety +2

    Boys boys

  • @christophermhina6548
    @christophermhina6548 Před 2 lety +1

    Bigger mind

  • @cdeleo9336
    @cdeleo9336 Před 2 lety

    Huyu kaka ni smart sana

  • @elimanase
    @elimanase Před 2 lety +4

    Huyu jamaa nimegundua leo anafanana sana na nikki wa pili

  • @jabarmalid5393
    @jabarmalid5393 Před 2 lety +1

    Kuna mtu anakumbuka kipindikileeee Salama anaflush CD choooni kama wimbo wako mbaya????🤣🤣🤣🤣🤣 tumetoka mbali sana.

  • @yurisongoro2895
    @yurisongoro2895 Před 2 lety

    Nilikua naisubiria sana hii kwakweli huyu nimtu muhim sana aisee

  • @dublinisa.isayamwinuka9657

    Huyu jamaa nimemuelewa sana

  • @ibrahimahead6133
    @ibrahimahead6133 Před 2 lety +1

    mjamaa yupo smart sana kwa kichwa

  • @jahadi5062
    @jahadi5062 Před 2 lety

    🥰🥰

  • @samsonnangai1286
    @samsonnangai1286 Před 2 lety +1

    Ningeshangaa na hatimaye Part1 hii hapa