RIPOTI MAALUMU|| HALI TETE MASOKO YA DAR, UKIUKWAJI WA SHERIA UKILETA MADHARA

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 6. 09. 2024
  • Utekelezaji usioridhisha wa sheria ndogo za masoko na za usimamizi wa mazingira katika Mkoa wa Dar es Salaam umesababisha kuwapo masoko yasiyo na viwango, miundombinu mibovu na uchafu unaohatarisha afya za wananchi.
    Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi kwa miezi mitatu kwenye masoko 11, umebaini sheria hazitekelezwi ipasavyo na kusababisha masoko mengi hali yake kuwa mbaya.
    Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya 2004, kifungu cha 115 (1), inahitaji mamlaka za Serikali za mitaa kufanya uchambuzi, utunzaji na utupaji wa taka kwa kuzingatia aina ya taka, kama za kuoza, plastiki, kioo au chuma. Hata hivyo, utekelezaji wake umekuwa wa kiwango cha chini.
    Hata uzingatiaji wa sheria ndogo za halmashauri kuhusu ushuru wa masoko na magulio, zinazohimiza kuboresha miundombinu, usafi na usalama wa masoko, hali haijakidhi viwango vinavyotakiwa.
    Kwa undani zaid wa ripoti hii maalumu, fuatilia kupitia tovuti ya Mwananchi na kwenye Chaneli ya CZcams ya Mwananchi Digital.

Komentáře • 2

  • @hajiabdalla5772
    @hajiabdalla5772 Před měsícem

    Tatizo sisi watu weusi wengi zarau hutujielewi wachafu

  • @bongo39
    @bongo39 Před měsícem

    Kipindupindu kitupu hawa viongozi wa mitaa wapo hapo kwa ajili ya kula tuu mitaani ndio hakufai diwani wapo lakini hamna kitu wabunge wapo watendaji wapo hii nchi sijui tufanye nini