REV. DR. ELIONA KIMARO: ELIYA, MTU ALIYEISHI NYAKATI MBILI

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 25. 07. 2024
  • KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH - IBADA YA MORNING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING - 07/11/2023.
    KICHWA CHA SOMO: KUSUDI LA KUWEPO"
    "A SENSE OF PURPOSE"
    NENO KUU
    UNAFANYA NINI HAPA?
    WHAT ARE YOU DOING HERE?
    NYI - KYIKYI UWUTA IHA?
    1 Wafalme 19 : 9
    ELIYA MTU ALIYEISHI NYAKATI MBILI
    ( OLD & NEW TESTAMENT )
    Malaki 4 : 4 - 6
    Luka 1 : 8 - 20
    Luka 9 : 28 - 36
    Mathayo 17 : 9 - 13

    Malaki 4 : 4 - 6
    4 Ikumbukeni torati ya Musa, mtumishi wangu, niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote, naam, amri na hukumu.
    5 Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na kuogofya.
    6 Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.
    Luka 1 : 8 - 20
    8 Basi ikawa, alipokuwa akifanya kazi ya ukuhani katika taratibu ya zamu yake mbele za Mungu,
    9 kama ilivyokuwa desturi ya ukuhani, kura ilimwangukia kuingia katika hekalu la Bwana ili kufukiza uvumba.
    10 Na makutano yote ya watu walikuwa wakisali nje saa ya kufukiza uvumba.
    11 Akatokewa na malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia.
    12 Zakaria alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia.
    13 Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana.
    14 Nawe utakuwa na furaha na shangwe, na watu wengi watakufurahia kuzaliwa kwake.
    15 Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.
    16 Na wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao.
    17 Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa.
    18 Zakaria akamwambia malaika, Nitajuaje neno hilo? Maana mimi ni mzee, na mke wangu ni mkongwe wa siku nyingi.
    19 Malaika akamjibu akamwambia, Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele za Mungu; nami nimetumwa niseme nawe, na kukupasha habari hizi njema.
    20 Na tazama! Utakuwa bubu, usiweze kusema, mpaka siku ile yatakapotukia hayo, kwa sababu hukuyasadiki maneno yangu; nayo yatatimizwa kwa wakati wake.
    Luka 9 : 28 - 36
    28 Baada ya maneno hayo yapata siku nane, aliwatwaa Petro na Yohana na Yakobo, akapanda mlimani ili kuomba.
    29 Ikawa katika kusali kwake sura ya uso wake ikageuka, mavazi yake yakawa meupe, yakimeta-meta.
    30 Na tazama, watu wawili walikuwa wakizungumza naye, nao ni Musa na Eliya;
    31 walioonekana katika utukufu, wakanena habari za kufariki kwake atakakotimiza Yerusalemu.
    32 Petro na wale waliokuwa pamoja naye walikuwa wamelemewa na usingizi; lakini walipokwisha amka waliuona utukufu wake, na wale wawili waliosimama pamoja naye.
    33 Ikawa hao walipokuwa wakijitenga naye, Petro alimwambia Yesu, Bwana mkubwa, ni vizuri sisi kuwapo hapa; na tufanye vibanda vitatu; kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya; hali hajui asemalo.
    34 Alipokuwa akisema hayo, lilitokea wingu likawatia uvuli, wakaogopa walipoingia katika wingu hilo.
    35 Sauti ikatoka katika wingu, ikisema, Huyu ni Mwanangu, mteule wangu, msikieni yeye.
    36 Na sauti hiyo ilipokwisha, Yesu alionekana yu peke yake. Nao wakanyamaza, wasitangaze kwa mtu siku zile lo lote katika hayo waliyoyaona.
    Mathayo 17 : 9 - 13
    9 Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu aliwaagiza, akasema, Msimwambie mtu ye yote habari ya maono hayo, hata Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu.
    10 Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, Basi kwa nini waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza?
    11 Naye akajibu, akawaambia, Kweli Eliya yuaja kwanza, naye atatengeneza yote,
    12 ila nawaambia, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, lakini wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu naye yuaenda kuteswa kwao.
    13 Ndipo wale wanafunzi walipofahamu ya kuwa amesema nao habari za Yohana Mbatizaji.

    Mhubiri : Mch. Dr. Eliona Kimaro
    Kwa maombi na ushauri :
    Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
    Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053

Komentáře • 5

  • @helenajoseph3182
    @helenajoseph3182 Před 8 měsíci

    Mungu dhihirika kwangu sasa niishi kwa kusudi lako hapa duniani

  • @itikabukuku7904
    @itikabukuku7904 Před 8 měsíci

    Amen.. Mungu akubariki mtumishi!! Ni kitu kimenisumbua sana

  • @rahabnkya8276
    @rahabnkya8276 Před 8 měsíci

    MUNGU ANA KUSUDI LA MIMI KUWEPO. MUNGU ATANIPIGANIA TU HATA NIMEMENENEWA MANGAPI. EEE MUNGU YAFITINISHE WATESI WOTE WAANGUKE NA WASIONEKANE TENA HIVI NOV DEC 2023. AMEEN.

  • @amosziro7054
    @amosziro7054 Před 8 měsíci

    Nimejengeka

  • @lisakuingwa7337
    @lisakuingwa7337 Před 8 měsíci

    Ninajambo la kufanyaa kabla ya sijafaaaaaa ..............kusudii la bwanaa bado lipo kwenye maishaaa