JUSSA: SIRI YA FEDHA ZA UVIKO/ZITO KABWE NDANI

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 12. 09. 2024
  • CHAMA cha act wazalendo kimesema kiongozi mkuu mstaafu wa chama hicho Zito Zuberi ruyangwa Kabwe ndie aliefanikisha Tanzania kunufaika na mkopo wa shilingi tirioni moja kutoka benki ya dunia na shirika la fedha duniani (IMF) ili kupunguza athari za kiuchumi baada ya kujitokeza kwa maradhi ya uviko 19
    Hayo yalielezwa na makamu mwenyekiti wa chama hicho Ismail Jussa Ladhu, alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika uwanja wa kata tango jimbo la Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba.
    mwenyekiti wa chama hicho tohaman masoud amesema wazanzibari wanapaswa kupigania mamlaka kamili ya nchi yao kwa vile ndio ukombozi utakaowaletea maendeleo na kuondoa tatizo la umasikini iwapo Zanzibar itapata mamlaka kamili.
    mjumbe wa kamati kuu wa chama hicho Seif Khamis, amesema katika kipindi cha miaka minne serikali imeshidwa kutekeleza ahadi zake ikiwemo kujenga bandari ya kisasa pemba na kuwainua wafajasiria mali kibiashara.
    Chama cha act wazalendo kinaendelea na mikutano ya hadhara kisiwani pemba ya jimbo kwa jimbo wakitumia muda mwingi kukosoa miradi ya serikali ikwiemo ya ujenzi wa masoko na barabara licha ya kuwemo kwenye serikali ya umoja wa kitaifa.

Komentáře •