REV. DR. ELIONA KIMARO: NITAKWENDA: I WILL GO ( NITAKWENDA YA YAKOBO)

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 25. 07. 2024
  • IBADA YA EVENING GLORY- THE SCHOOL OF HEALING - MAFUNGO YA SIKU 40 - 23/03/2023 - SIKU YA 24
    SOMO : "NITAKWENDA"
    "I WILL GO"
    NENO KUU
    Luka 15:18
    18 Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako;
    Isaya 6:8
    8 Kisha nikaisikia sauti ya Bwana, akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, Mimi hapa, nitume mimi.
    UJUMBE WA LEO: NITAKWENDA YA YAKOBO
    (UNA KITU CHA KUFANYA KABLA HUJAFA)
    Mwanzo 45 : 25 - 28
    Mwanzo 47 : 7 - 12

    Mwanzo 45 : 25 - 28
    25 Wakatoka Misri, wakafika nchi ya Kanaani kwa Yakobo, baba yao.
    26 Wakampasha habari, wakisema, Yusufu angali hai; naye ndiye mtawala katika nchi yote ya Misri. Moyo wake ukazimia, kwa sababu hakuwasadiki.
    27 Wakamwambia maneno yote ya Yusufu, aliyowaambia; na alipoona magari aliyoyapeleka Yusufu, ili kumchukua, roho ya Yakobo baba yao ikafufuka.
    28 Israeli akasema, Yatosha! Yusufu mwanangu angali hai; nitakwenda, nionane naye kabla sijafa.
    Mwanzo 47 : 7 - 12
    7 Yusufu akamleta Yakobo babaye ndani akamweka mbele ya Farao Yakobo akambariki Farao.
    8 Farao akamwuliza Yakobo, Je! Siku za miaka ya maisha yako ni ngapi?
    9 Yakobo akamjibu Farao, Siku za miaka ya kusafiri kwangu ni mia na thelathini; siku za miaka ya maisha yangu zimekuwa chache, tena za taabu, wala hazikufikilia siku za miaka ya maisha ya baba zangu katika siku za kusafiri kwao.
    10 Yakobo akambariki Farao, akatoka mbele ya Farao.
    11 Yusufu akawakalisha babaye na nduguze, na kuwapa milki katika nchi ya Misri, katika mahali pazuri pa nchi, katika nchi ya Ramesesi, kama Farao alivyoamuru.
    12 Naye Yusufu akawalisha babaye na nduguze na nyumba yote ya babaye, kwa kadiri ya hesabu ya watoto wao.

    Mhubiri: Rev. Dr. Eliona Kimaro
    Kwa maombi na ushauri:
    Mch. kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
    Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053

Komentáře • 4