NEEMA YA MUNGU HUJA NA TAARIFA (I) - PASTOR SUNBELLA KYANDO

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 5. 09. 2024
  • Kabla ya tatizo lolote kutokea Mungu huachilia taarifa ndani ya mtu.Watu wengi wamekuwa wakiingia kwenye matatizo kwa sababu ya kutosikiliza sauti ya Mungu.Mungu huachilia neema yake ili janga linalotakiwa kutokea lisikupate na wewe unatakiwa ufanyie kazi maelekezo yote anayokupa.Favour(Kibali) bila information ni rahisi sana ukaishia kwenye mauti.
    Leo hii ukiuliza watu wengi waliopata ajali watakwambia kuwa kabla hawajaanza safari walisikia uzito ndani yao, Mungu aliwazuia lakini kwa sababu za kibinadamu wakalazimisha kwenda na matokeo yake wakapata ajali.Hata kama premature death sio sehemu yako lakini pia una nafasi yako ya kufanya.Hata pia walioingia kwenye ndoa zisizo sahihi watakwambia kabisa kuwa Mungu aliwaonya mapema kabisa.
    Nuhu baada ya kupewa maelekezo na Mungu ya kutengeneza safina alitii, Mungu hakuishia hapo akampa maelekezo juu ya nani na nini vinatakiwa kuingia kwenye hiyo safina na akamwambia kuwa kila wanyama,ndege,wadudu na kila kiumbe kitakachoingia kwenye safina ahakikishe ni dume na jike,kwanini? kwa sababu wakiwepo dume na jike kwenye safina kuna uhakika wa uzao(ongezeko) .Yaani ndio najua Nuhu tayari kuna maono unayo lakini kuwa makini sana na watu unaowaingiza kwenye safina yako,ingiza watu watakaoweza kuzalisha kile kitu kilicho ndani yako,watu watakaoleta ongezeko kwenye maono uliyonayo.Na kutokana na kutii kwa Nuhu leo hii vitu vyote,ndege na wanyama wote walitokana na wale ambao Mungu alimwambia Nuhu awahifadhi kwenye Safina.Utii wako kwa Mungu ndio ongezeko lako lilipo.

Komentáře • 71