Vatican News Watilia Mkazo Tamko la Maaskofu Kuhusu Bandari, Hatuungi Mkono, Watu Wasikilizwe

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 6. 09. 2024
  • 𝐖𝐄𝐙𝐄𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐓𝐔𝐌𝐄 𝐖𝐀 𝐉𝐔𝐆𝐎 𝐌𝐄𝐃𝐈𝐀 𝐊𝐔𝐏𝐈𝐓𝐈𝐀 𝐌-𝐏𝐄𝐒𝐀 𝐋𝐈𝐏𝐀 𝐍𝐀𝐌𝐁𝐀 𝟓𝟎𝟓𝟒𝟔𝟑𝟓 𝐉𝐈𝐍𝐀 𝐉𝐔𝐆𝐎 𝐌𝐄𝐃𝐈𝐀 𝐍𝐄𝐓𝐖𝐎𝐑𝐊
    Ijumaa tarehe 18 Agosti 2023, Baraza la Maaskofu Katoliki Nchini Tanzania (TEC) limetoa tamko la kupinga mkataba wa usimamizi na uendelezaji wa bandari za Nchi uliosainiwa kati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania na Nchi za Falme za Uarabuni huko Dubai na kuridhiwa kupitia azimo la Bunge mnamo tarehe 10 Juni 2023, huku wakifafanua kwa kina jinsi ambavyo mkataba huo haukubaliki kwa watanzania wengi, tangu kuanza kwa mjadala. Tamko hilo limesainiwa na Maaskofu wakuu na maaskofu wote 37 wa Majimbo Katoliki Tanzania ambapo kabla ya kukabidhiwa kwa Mkataba huo kwa waandishi wa Habari, imetangazwa kwa umma na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Mheshimiwa Padre Charles Kitima kwa vyombo vya Habari
    Kwa upande wake Padre Kitima amesema Maaskofu hawaungi mkono bandari kuwekwa chini ya mwekezaji mmoja na kwamba tamko hilo la Maaskofu lina kauli moja ambayo ni kwamba “kama wananchi hawautaki mkataba, serikali iwasikilize wananchi. Serikali iachane na Mkataba wa Bandari kwa sababu wananchi wamegawanyika kuhusu mkataba huo na zaidi ni kutokana na vifungu flani fulani ambavyo haviendani na Katiba ya Nchi na matakwa ya raia”. Hata hivyo hii siyo kwa mara ya kwanza sauti ya Viongozi wa kidini kusikika, hata siku zilizopita waliweza kutoa maoni yao na sio viongozi wakatoliki tu, lakini hata wa makanisa mengine na madhehebu mbali mbali kupitia mijadala.
    Mjadala juu wa uwekezaji unaotarajiwa katika usimamizi wa bandari za Tanzania umedumu tangu mwanzoni mwa mwezi Juni 2023 huku kukiwa na mitazamo tofauti kati ya wanaounga mkono na wanaopinga. Na hii ilisababishwa na kukosekana muda wa wanachi wote kupewa fursa zaidi ya kuadili. Na siku za hivi karibuni, baadhi ya wanasheria, walipeleka hata mashtaka, katika mahakama ili kutaka haki za wananchi, lakini hatimaye wakaishia kuwekwa ndani, ambapo wameachiliwa huru tarehe 18 Agosti 2023. Katika muktadha wa haki za binadamu (Amnesty International), hivi karibuni lilinaomba: “waachilie mara moja Wakosoaji waliozuiliwa wa mkataba wa bandari nchini Tanzania.
    Tanzania:Amnesty International inaomba waachiliwe wakosoaji wa mkataba wa bandari
    Hawa ni Dk. Willibrod Slaa, aliyekuwa mbunge na Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Boniface Mwabukusi, mwanasheria na mwanaharakati, na Mdude Nyagali, mwanaharakati wa kisiasa, ambao wote walikamatwa kati ya 12 na 13 Agosti 2023, kwa kosa la kukosoa makubaliano kati ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), kuhusu bandari”. Hayo yalisemwa na Shirika la Amnesty International mnamo tarehe 14 Agosti 2023, kupitia kwa msemaji wake Tigere Chagutah, Mkurugenzi wa Kanda ya Amnesty International ya Afrika Mashariki na Kusini.
    Kwa mujibu wake alisema “ Makubaliano hayo yanaweka mfumo wa kisheria kwa UAE kushirikiana na Tanzania katika maendeleo, usimamizi na uendeshaji wa bandari za Tanzania, kanda maalum za kiuchumi, mbuga za usafirishaji, korido za biashara na miundombinu mingine inayohusiana nayo. Ukandamizaji wa mamlaka ya Tanzania dhidi ya wakosoaji wa mpango wa bandari ya UAE unaonesha kuongezeka kwa kutovumilia kwao upinzani. Kwa hiyo Mamlaka lazima ziache kuwashikilia wanaharakati kiholela kwa sababu tu ya kutoa maoni yao kwa amani na kuwaachilia mara moja na bila masharti wanaharakati hawa ili kuhakikisha kuheshimiwa kwa haki ya uhuru wa kujieleza.” Alisisisitiza Tigere Chagutah.
    Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican, inakutleta Hati nzima ya Tamko la Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania iliyopchapishwa tarehe 18 Agosti 2023:
    Follow this link to join my WhatsApp group: chat.whatsapp....
    Tumsifu Yesu Kristo, Napenda Kukushukuru kwa Kuwa Mdau Mpendwa wa Jugo Media. Tunapenda kukutaarifu kuwa Tumeandaa Group Maalum kwa Ajili ya Kupokea Taarifa Mbalimbali za Kanisa, Misa Live, Vipindi vya Kanisa nk kutoka Jugo Media. Kama ungependa Kuungana Nasi Tunaomba Ujiunge kwa Hiari Kupitia Link Hiyo Juu. Mungu Akubariki Daima
    KAMA UNGEPENDA KUPATA TAARIFA KUHUSU KANISA KWA NJIA YA WHATSAPP TAFADHARI TUMA UJUMBE KWA WHATSAPP UKISEMA NIUNGE KISHA JINA LAKO KWENDA NAMBA +255757560764 au BONYEZA LINK HII wa.me/+2557575...) (SAVE HII NAMBA KWANZA, ANDIKA JUGO MEDIA) UBARIKIWE SAMA
    KAMA UNA HABARI NA UNGEPENDA KUSHIRIKI PAMOJA NASI TAFADHARI WASILISHA KUPITIA WHATSAPP NO +255757560764 AU BONYEZA wa.me/+2557575...)
    Tafadhali Subscribe, Like, Comment na Share tone hili la upendo kwa ndugu jamaa na marafiki.
    𝐉𝐮𝐦𝐮𝐢𝐤𝐚 𝐧𝐚𝐬𝐢 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐦𝐢𝐭𝐚𝐧𝐝𝐚𝐨 𝐦𝐢𝐧𝐠𝐢𝐧𝐞 𝐲𝐚 𝐊𝐢𝐣𝐚𝐦𝐢𝐢:
    Instagram: / jugo_media
    Facebook: / jugomedia2019
    𝕄𝕒𝕨𝕒𝕤𝕚𝕝𝕚𝕒𝕟𝕠:
    JUGO MEDIA,
    Sokoine Drive, Posta
    P. O. BOX 34014,
    Dar es Salaam.
    For Bookings and other Enquiries
    Phone Number +255757560764/657790405
    #jugomedia #kanisakatoliki #familiatakatifu #wawata #uwaka #viwawa #australia #unitedstates #canada #america

Komentáře • 279

  • @marialesulie6798
    @marialesulie6798 Před rokem +13

    👏👏👏👏Asanteni kwa kuitetea nchi yetu kwa uzalendo wa kweli

    • @brunomchalla4439
      @brunomchalla4439 Před rokem

      Hongera Maaskofu wa Kanisa Katoliki kwa Hekima yenu kuwasemea Watanzania wanaoishi kama watumwa.

    • @brunomchalla4439
      @brunomchalla4439 Před rokem

      Nashauri pia,Jumuiya zote za Kanisa zisambaziwe Waraka huu waelewe ubovu wa mkataba, badala ya propaganda zinazo utetea.

    • @shabanbaheza4711
      @shabanbaheza4711 Před rokem

      Xyo uzalendo Bali ni maslah yao na kanisa tu

    • @shabanbaheza4711
      @shabanbaheza4711 Před rokem

      ​@@brunomchalla4439hii nchi ni ya makanisa wezi wakubwa mmezoea maruzuku hakuna 😂😂😂😂 hayo ni maslah tumeelewa, hao wananchi mnawasemea lkn sis wananch tunajitambua sis tupo na serikal nguvu moja kama kweli hawa niwakweli mbn hawajaandika waraka kupinga ushoga mbwa nyie

  • @gracewilly5143
    @gracewilly5143 Před rokem +13

    Jamani maasikofu asanteni kwa ukombozi mmetukomboa wananchi asanteni mungu wabariki wote maasikofu

  • @user-hq3ld9nk8n
    @user-hq3ld9nk8n Před rokem +10

    Tunawapongeza tec kwa kutusemea watanzania masikini na mafukala mungu awabariki nyinyi ni mabarozi wa mungu

  • @user-to2vq5xy3h
    @user-to2vq5xy3h Před rokem +7

    Maaskofu wote mbarikiwe kwa kutuombea tanzania yahamani mbarikiwe sanatu

  • @wilsonjeremia7894
    @wilsonjeremia7894 Před rokem +10

    sisi ni wanyonge msipo tusemea ninyi sisi hatutakuwa salama, asanteni sana mababa askof kwa mioyo yenu ya huruma kwetu,

  • @anosiata8242
    @anosiata8242 Před rokem +10

    Mungu awarinde maasikofu kwa kutetea rasimali zetu

    • @KaburuKimath-eu5nf
      @KaburuKimath-eu5nf Před rokem

      Nilikuwa nimekata Tamara na kanisa Sasa naanza kuwa na Imani na na aaza kurudi kanisani Kwa adabu zote

    • @anosiata8242
      @anosiata8242 Před rokem

      @@KaburuKimath-eu5nf ni vizuri kwenda kumuomba mungu

  • @user-kx5ht4ov6o
    @user-kx5ht4ov6o Před rokem +8

    Amina maaskofu wetu.

  • @FurahaRogers-qw1ch
    @FurahaRogers-qw1ch Před rokem +7

    Maskofu wetu tunawashuru sana mubalikiwe

  • @drallan6879
    @drallan6879 Před rokem +1

    Maaskofu tuteteeni CCM Wana maslahi binafsi mkataba ni mbovu mno;u will be blessed over this!

  • @NgambilabalinziBaliguluk-os3ln

    Ahsante Sana MUNGU Akubariki Baba Padre Tuko nyuma yenu

  • @StevenGendo-vx9jo
    @StevenGendo-vx9jo Před 11 měsíci

    Mwenyez mungu awabarik nakuwalinda maaasikofu wetu wote wanaopambania rasilimali zetu.

  • @aloycemisigalo3983
    @aloycemisigalo3983 Před rokem +1

    Cc wananchi wa Tanzania tumefurahi sana kwa uamuzi wa kanisa kuu Katoliki kwa kutupazia sauti cc wananchi, Kanisa Katoliki limeonesha ukomavu mkubwa kwa kutupazia sauti cc tusio kuwa na sauti, hongereni sana maaskofu wasomi wa Kanisa Katoliki.

    • @shabanbaheza4711
      @shabanbaheza4711 Před rokem

      We ni mwanachi au kafir 😂😂😂😂😂😂😂mbwaa ww

    • @acquelinapissa2968
      @acquelinapissa2968 Před 11 měsíci

      @@shabanbaheza4711tulia na mkeo huna unachokielewa acha wanaume watanzania waongee we uweze kuendesha nyumba yako

  • @WediMwamahonje-eb3dh
    @WediMwamahonje-eb3dh Před rokem +1

    Asante Sana maaskofu wa dini la katoliki,kkkt mnajificha kwa nn mnataka nn kupitia hili la bandari

  • @francissimwinga-gb2vd

    Amina hawatafaniwa juu ya Mali zetu za nchi

  • @boniphacesholla4433
    @boniphacesholla4433 Před rokem +2

    Amina katoriki .

  • @angelsulle7177
    @angelsulle7177 Před rokem +5

    Doctorate ya maaskofu wetu ni ya kusomea so ya kupachikwa kama ya hao wengine wanao soi soi TEC wametingishaaa!!!! Hongereni Baba zetu nyuma yenu sisi

    • @camilluskassala8362
      @camilluskassala8362 Před rokem

      Wimbo wetu wa Taifa unatukumbusha kuwa hekima ni ngao yetu ya kwanza!

  • @CanonLuhunga-oc9sx
    @CanonLuhunga-oc9sx Před rokem +6

    Mwl aliwahi kusema Wazanzibari wakijitenga, Watanganyika watabaki wameduwaa , hata Mimi nimeduwaa niwe sehemu ipi , lakini serikali kweli imekosea? hebu wakae pamoja waonyeshane penye wasiwasi waelewane Nina wanangu nawapenda mno wanangu

  • @floramote6939
    @floramote6939 Před rokem

    Amina baba zetu

  • @husnapeterkisiri2072
    @husnapeterkisiri2072 Před 11 měsíci

    Amina baba zangu

  • @petrochonya4582
    @petrochonya4582 Před rokem +2

    Safi sanaaaaa

  • @silviangowi6634
    @silviangowi6634 Před 11 měsíci

    Amina

  • @trillhappybeautypoint9874

    Asnteni baba Maaskofu

  • @BlandinaMassawe
    @BlandinaMassawe Před rokem

    Asante mungu tungekuwa watumwa wa shetani tungefan,ishwa kazi kama babu zwtutungeuzwa mnadani km mbuzi ĥ

  • @kakasayohana637
    @kakasayohana637 Před rokem

    😂😂😂🎉🎉🎉❤❤❤nimeipenda hiyo na imepita watanzania tumelogwa na hata hao baadhi ya viongozi wa dini wanafki walishindwa hata kuikosoa serikali wakawa wanaponda waraka huo tec wakombozi tumepigwa sana.sasa kilicho baki ni mapinduzi tumechoka

  • @FrankMwaiswasu-dt5ey
    @FrankMwaiswasu-dt5ey Před 11 měsíci

    Hongo mbaya pamoja na kelele hizi za wananchi hawataki kuzitapika wameshupaza shingo zao

  • @rosetreffert4179
    @rosetreffert4179 Před rokem +2

    Amina Amina ❤❤

  • @SanaiKiruki-db3nf
    @SanaiKiruki-db3nf Před rokem +1

    One broad question is how we achieve particularization of our identity as one nation with competing antimonies for change trajectories: politics, economy, media, science, law, religion as far as globalisation is concern on debate on value for de-regulation with modern Tanzania investment and foreign policy

  • @marialesulie6798
    @marialesulie6798 Před rokem +8

    God bless you bishops. You are really true patriotic. Mmeonesha uzalendo wa kweli wa hali ya juu kwa taifa lenu

  • @festokemibala5832
    @festokemibala5832 Před rokem +1

    Farao alijifanya mbabe kutotii sauti ya mungu kupitia mtumishi wake Musa. Kilichomkuta wale wasomaji wa biblia wanajua, ni mapigo kumi ya haja! Viongozi tuepushe na hasira za mungu wa kutotii sauti yake

  • @Ibnimohd-tr6qc
    @Ibnimohd-tr6qc Před rokem +1

    Ahsanten maaskof na nyinyi kwa kuafata mkumbo!! Sawa na nyie ndo mshaskilkana! Ila muje tu kelele za chura hazimsababishi tembo kunywa maji!!! Mama endelea msumari ushawaingia ao!!! Apo apo!! Mpk tukamilishe mkataba!!!!

  • @yahyadenny4368
    @yahyadenny4368 Před rokem +1

    Eti watanzania wengi hawataki uwekezaji wa bandari toeni takwimu acheni uongo mapunda haya .

    • @user-gv9zo3os2m
      @user-gv9zo3os2m Před rokem

      Hizo kauli zako mkristo hawezi kuzitoa. Ina maana unamkisoa Mungu aliyewaimba. ikiwa wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu pia nawewe umeumbwa kwa mfano wa Mungu basi na wewe ni punda umejitukana indirect.Elimu ni ya muhimu sana kwetu.Unapotoa hoja toa hoja yenye mashiko hatimaye utamtukana muumba wako bila kujua mwishowe itakula kwako. Pole sana na hongera kwa k
      Malezi mabovu.Mimi binafasi siwezi kwa binadamu yeyote yule

  • @GozbertAliseni-vp6kj
    @GozbertAliseni-vp6kj Před rokem

    Mungu.awabariki

  • @emmanuel_mangula
    @emmanuel_mangula Před rokem

    Tunajivunia kuwa ninyi Maaskofu wetu wote Asanteni saana na mmbarikiwe saana🙏🙌

  • @user-zz3wm3nf1j
    @user-zz3wm3nf1j Před 11 měsíci

    Inauma sana ila tu tumwachie mungu,ila tunawashuru sana viongozi baadhi mnao tusemea,mungu awasaidie sana,asntn

  • @deborahmgedzi632
    @deborahmgedzi632 Před rokem +3

    Amina Amina Amina

  • @safisimkoko1932
    @safisimkoko1932 Před rokem

    Eee mwenyezi MUNGU tusaidie DAIMA utudumishie AMAN UPENDO NAUTURIVU amen

  • @Mhandisi2008
    @Mhandisi2008 Před rokem

    Inahitaji jicho la mbali sana kufahamu huu mkataba haufai, vizazi vijavyo vitatulaumu sana...

    • @omaryjudasymwanga7172
      @omaryjudasymwanga7172 Před rokem

      Upo sahihi Angalia loliondo wale masai wanakipata sema hawana platform ya kusemea it's sad lakini pangepatikana watu ambao hawakula hela ya muarabu wakaenda kufanya enterview na wale masai mngejua madhila ya wale jamaa pale juu wanayopitishwa na wale Waarabu nimsala sema wanaotumwa ulikula hela ya hao watu so wanawakingia kifua ili laana isiwarudi lakini jiulizeni nani analaaniwa Kati ya mtu anayeuza utu wa watu wake au aliyepewa chakula na mgeni na kuogopa kusema ajili ya kipande cha mkate mtakua ndani ya laana ambayo haitakwisha kama ilivyo sasa damu za masai zinavyomwagwa kwa kuingilia kipande alichopewa muarabu mnauwa wa kwenu mnaremba wa jirani aloo mungu awasimamie kweli njaa nimbaya mtakula lakini baada ya.kula mtakufa hakika mungu hadhihakiwi msimuonee mnyonge

  • @samakisamaki3226
    @samakisamaki3226 Před rokem +3

    Samia ndiye aliyesaini. Samia anajua kuwa 2025 hatoboi, anatafuta chake mapema 2025 akaishi marekani kwa ustawi wake

  • @samwelyesaya1202
    @samwelyesaya1202 Před rokem +3

    Hapo nawaunga mkono mko sahihi mkataba huuni mbovu kwa nini unalazimishwa na serikali

  • @wilsonjeremia7894
    @wilsonjeremia7894 Před rokem +5

    ATUKUZWE MUNGU MILELE NA MILELE

  • @omaryjudasymwanga7172
    @omaryjudasymwanga7172 Před rokem +1

    Njaa ni mbaya sana hawa viumbe wanaharibu nchi ajili ya njaa ya siku moja

  • @venerandaaloyce1947
    @venerandaaloyce1947 Před rokem +4

    Maaskofu wapewe mauayao❤❤

  • @Mohamedkitulu
    @Mohamedkitulu Před rokem +1

    TAKIBIIIIII

  • @rosetreffert4179
    @rosetreffert4179 Před rokem +1

    ❤❤❤❤❤❤🎉

  • @michaeljumanne5921
    @michaeljumanne5921 Před rokem +1

    Hawa maaskofu wa kanisa Katoliki hawana hata chembe ya kuwasemea watanzania juu ya utawala wa inchi. Mungu sio wa kwao peke yao ni wa wote.

    • @marialesulie6798
      @marialesulie6798 Před rokem +1

      Na rasilimali ni za watanzania wote na wao ni sehemu ya watanzania. Lazima wakemee uovu kwenye jamii zetu kama viongozi wa kijamii na kiroho pia. Hiyo ndiyo kazi yao haswaaa.

    • @marialesulie6798
      @marialesulie6798 Před rokem +1

      Tungewashangaa sana kama wangekaa kimywa wakati wao ni sehemu ya jamii yetu na ambao hata wao mkataba huu unawahusu kwa kweli wangetuudhi sana. Wao ni sehemu ya jamii yetu na viongozi wetu wa kimaadili. Lazima wakemee uovu na kukosoa pale maadili yanapokiukwa….hiyo ndiyo kazi yao haswa katika jamii zetu.
      Viongozi wa serikali nao ni wanajamii hii hii na maadili yanawahusu. Huelewi nini hapo?

    • @marialesulie6798
      @marialesulie6798 Před rokem

      Na nchi hii siyo ya wengine bali ni ya kwao pia. Ni ya ndugu zao na jamii zao. Tumepewa wote na Mungu tuilinde kwa pamoja. Huelewi nini hapo?

    • @annasolomon9855
      @annasolomon9855 Před rokem

      ​@@marialesulie6798nimewapenda Sana maaskofu wa katolik , sio yule Mzee wa upako aliyepewa bahasha 😊😊

  • @twalibkabota6249
    @twalibkabota6249 Před rokem

    Tatizo ninyinyi hamuwaambii watanzania wamshindwa kujisimamia maguful wamemuona mbaya alipowafunza hayo akiwamteule mpakwa mafuta aliekula nanyi karam mbalmbali ,nanyimkamkana gorigota kimyakimya ,mamakapewa msaraba mnamwambia arudi misr kwenye mkate ,mama wawatu akiwanamsalaba ndani yasafa katkat maski naakumbuka anakubar ajitutumua ageuke ndokanun ndani yask tat tatu 🙏misr ili wamwelewe arudi anabedha ndowatoto wale sasa mtanzania usalama upiwewe unafata mkumbo dunia moja ,usarama uchumi mtuanakupiga akiwa chumbani wee acheni mama afanye maajab kamandoa inavunjika sembuse mkataba bubirin mwarab amwage hela wanahela awooo mzungu anajua nanyimpeni moyo ,mkimkera sana mana ajawambia anashida saana naurahis mpaka kuuwa watu atawaachia atawachia nalaana yakuachiwa ukichanya na hii hili taifa utapigwa laana heee toen matamko kama haya kwakuomba nakufunga wanasiasa ni michezo uhalisia nitifauti ,kwahaya naimani mtakanusha bakusimama unapostahil shalomshalom

  • @AW-vt9pw
    @AW-vt9pw Před rokem

    Sio wananchi semeni Maaskofu

  • @yahyadenny4368
    @yahyadenny4368 Před rokem +1

    Ona yamevaa majoho mekundu ishara ya kuua.ueni tu hivi punde mtakiona za mtema kuni.

  • @user-cd9re4wt2b
    @user-cd9re4wt2b Před rokem

    Mmefanya vizuri kutounga mkono mkataba Mbovu

  • @benedictoshadrack2573
    @benedictoshadrack2573 Před 11 měsíci

    Kiukweli huo mkataba hatuutaki kabisa kwa nn wanalazimisha inchi hii siyo ya mtu mmoja au kikundi cha watu badala yake ni inchi ya mamilioni ya watu wengi ambao niwanainchi wenyewe pia

  • @marialesulie6798
    @marialesulie6798 Před rokem +2

    Siyo nchi za jumuiya ya falme za kiarabu bali kampuni dpw ya Dubai.

  • @omaryjudasymwanga7172
    @omaryjudasymwanga7172 Před 11 měsíci

    Nikipofu na mwenye mtindio wa uwezo wa kufikiri pekee ndiye atakubali hili maana hajui Kati ya nyeupe na nyeusi so jaribuni kuchambua kabla yakuweka saini za makubaliano maana nyie kua mbele haimanishi mnaakili kuwazidi wengine au mnaona mbele zaidi so nivyema maswala ya nchi yakazingatia katiba na sio vile mtu mmoja au kakikundi flani kanataka basi iamuliwe kua sheria hiyo sio sawa

  • @user-rc1dp6ux3k
    @user-rc1dp6ux3k Před 11 měsíci

    Hakuna nchi duniani ambayo ilishawahi kuendelezwa na wageni

  • @user-jz6dd8cj8s
    @user-jz6dd8cj8s Před 11 měsíci

    Binafsi na amini, kila kitu kitakuwa sawa, maana nchi niyetu, but rais samia afahamu kuwa nchi hii ni nchi ya wananchi au watanzania, hasilazimishe

  • @danielshauri6390
    @danielshauri6390 Před rokem +3

    SERIKALI ILIPASWA KUSEMA
    MITAMBO YA KISASA YAKUIFANYA BANDARI KUWA YA KISASA ,,NA YENYE UFANISI , NI KIASI GANI ???
    ILI TUONE KWAMBA KWELI SISI KAMA TAIFA HATUZIWEZI HIZO GHARAMA .
    NDIPO TUSHAWISHIKE KUONA KWAMBA KWELI TUNAHITAJI MUWEKEZAJI.
    HALAFU TUWEKE MIKATABA YENYE FAIDA KWA TAIFA , SIO HII YA HASARA

    • @sabraham5308
      @sabraham5308 Před rokem

      wazungu/wakristo ndio mnaowafanya mabwana zenu,mwadui minning wanaichukua almasi/dhahabu mpaka leo,toka uhuru wamekabidhiwa wakoloni hawa watunyonye mpaka leo,msitubabaishe wakatoliki,nchi haina dini,nyinyi mna ubalozi Vatican,waislamu wanazuiliwa wasijiunge na jumuiya ya kiislamu ya ulimwengu OIC,haya tuyajadili,ni mengi tunayo,msituchokoze

    • @marialesulie6798
      @marialesulie6798 Před rokem

      Uko sahihi kabisa

  • @user-mm9mq8db1d
    @user-mm9mq8db1d Před rokem

    Mungu tutetee wana wako kwakweli

  • @rosetreffert4179
    @rosetreffert4179 Před rokem

    ❤❤

  • @salminsomba2491
    @salminsomba2491 Před rokem +1

    Wapi wa Tanzania wengi wamsema hautaki huo mkataba bali ni kanisa katoloki tu ndiyo hamuutaki msiiwaingize watanzania tunaomba watoe ushahidi wapi watanzania wasema hawataki kwahiyo hao watanzania ambao hawataki baraza la wakatoliki ndilo linawasemea hao watanzania ambao hawataki? Baraza liweke wazi kuwa varaza ndiyo wakili wa watanzania kupinga huo mkataba ? Lakini baraza litoe idadi ni asilimia ngapi ya watazania imekataa ili tuone wingi wao Hilo tamko la baraza linaonekana hapo baraza ndilo linataka kuipangia serikali ifanya hilo wanalotaka wao naunga mkono mzee wa upako huyo ni askofu wa kweli Tanzania amezungumza ukweli kuhusu huo waraka wa maaskofi mkristo mwenzao ansema ukweli kuwa waraka huo ni wa maslai binafsi ya baraza tunaomba baraza lijikite kwenye dini tu wasijuchanganye na siasa wataleta vurugu sasa tunaomba kila taasisi ya dini itoe waraka alafu tuone maamuzi ya taasisi zingine wataamua nini baraza la maaskofu wanaposema rais afute huo mkataba maana yake tayari baraza limeishatoa hukumu na kumtaka rais afute katika taasisi za kidini nchini ni nyingi kwanini kelele nyingi zinapigwa na baraza la wakatolikii? TCS walikuwepo hapa kwa miaka 25 baraza lilikaa kimya je baraza linaweza kutueleza faida ambayo nchi ilipata kupitia TCS ? Tumechoka kusikia kelele za baraza hilo

    • @marialesulie6798
      @marialesulie6798 Před rokem

      Wewe nawe inaonekana hauko Tanzania au siyo mwananchi maana dah! Yaani Hivi vilio vyoooote hata kwenye mitandao napo huoni kweli? Da ama kweli sikio la kida halisikii dawa.
      Tunakusamehe bure maaana huelewi

    • @marialesulie6798
      @marialesulie6798 Před rokem

      Wewe vipi?
      Kwani inachopinga ni nini hasa?Baraza wametoa waraka kusomwa hata wiki haijapita. Mbona Watu wengi wakowemo wachumi wakubwa na wanasheria wabobezi wameongea kuanzia day one mkataba ulipovuja au wewe haikuwa unaangalia hata vyombo vya habari? Mbona hata mahakama kuu mbeya majaji wamezungumza? Mbona hata mkutano wa sauti ya watanzania na Chadema kule mbagala wamezungumza sana toka mwanzo kabisa? Kwani wewe inaishi wapi ambako hata mitandao huwezi kuona? Shoda yake ni baraza la wasomi mangili maaskofu au ni jambo jingine?
      Shida yako ni waraka na ujumbe iliomo ndani au ni watoa waraka unawachukia? Ujue hata wao ni watanzania wananchi hii ni yao pia wana haki zote kikatiba kukosoa au kutoa ushauri pale inapobidi. Huwezi kuwazuia hata kama unawachukia bila sababu ya maana.

  • @emmanueltuppa5459
    @emmanueltuppa5459 Před rokem +1

    💪💪💪💪💪💪🙏🏼🙏🏼🙏🏼

  • @EdgaKatare-xp6rj
    @EdgaKatare-xp6rj Před rokem +1

    Nami naungana

  • @issaabdi9129
    @issaabdi9129 Před rokem +1

    Ni wanafi tu wanekosa mahali pa ulaji. Dp world inasimamia hata bandari ya uingereza na nchi krb 50.acheni ulofa

  • @kiatu
    @kiatu Před rokem +4

    Maaskofu ni WASOMI na wakweli popote duniani, si WAOGA?

  • @user-xb7iy9mr6w
    @user-xb7iy9mr6w Před 11 měsíci

    Kweli kabisa mkataba huu hatuutakii ila serikali imeshupaza shingo yake.

  • @johanesrwemela5250
    @johanesrwemela5250 Před rokem +1

    Nakupata katika ubora wako

  • @yahyadenny4368
    @yahyadenny4368 Před rokem +1

    Walimshauri Magufuli aibe na kuchukua fedha za wafanya biashara kwa nguvu kwa kosa hilo wakamsababishia madhara makubwa.Yote hayo tunayajua farasi majike .

    • @user-gv9zo3os2m
      @user-gv9zo3os2m Před 11 měsíci

      Toa hoja usikurupuke kama ni msomi toa kisomi kama la achia ngazi kaa pembeni. Matusi si utamaduni wa wakristo hatujafundishwa hivyo.

    • @alphonceassenga2843
      @alphonceassenga2843 Před 11 měsíci

      Aisee wewe jamaa una shida sana.

  • @user-cy1zu3zq8v
    @user-cy1zu3zq8v Před 11 měsíci

    Yote kwa mungu

  • @SanaiKiruki-db3nf
    @SanaiKiruki-db3nf Před rokem

    Enhancing strategic security is very significant role to maintain our status quo and public image, With inside matters and outside matters to our situational analysis: opportunities, strengths, weakness and threats with political man decision or economic man decision criteria wise: Content Analysis, Cost-Benefit Analysis, Regression Analysis, Break-Even Analysis, SWOT Analysis, Marcov Analysis, User-Based Analysis, Management by Objectives (MBO), Range Solution and Grade Flexibilities, as far as Operational and Strategic risk plan on four questions are concern: Financial, Customer Goal, Internal Efficiency and Learning Organization

  • @fransiskamwinuka4750
    @fransiskamwinuka4750 Před 11 měsíci

    Kwa mtu. Asiye na shule kichwani ndiye atakayeshabikia huu mkataba, lakini kwa mtu ambaye ameingia darasani na elimu yake ya kutosha hawezi kuushabikia huu mkataba. Shida iliyopo hapa shule hakuna kwa walio wengi ndio maana kila ki2 ndioooooo hata kama hakina manufaa kwao. Shida sana. Nenda kafute ujinga uliopo kichwani kwako ili ujue baya na zuri. Watanzania wengi akili ndogo.

  • @SanaiKiruki-db3nf
    @SanaiKiruki-db3nf Před rokem

    Tumlindie mama Heshima yake na Imani ya kuliongoza taifa letu

  • @jumakapilima7295
    @jumakapilima7295 Před rokem +2

    Hata wafike wapi, janjajanja zao kupitia bandari zinakwenda kwisha! We support Madame President, we support Dar Port investment by DP world for a better future of our country!! Kazi iendelee!!

    • @PascalPascual-rn6fx
      @PascalPascual-rn6fx Před rokem +1

      Pole sana. Hamutakaa mfanikiwe.

    • @THADEOCHUNDU-eu3ez
      @THADEOCHUNDU-eu3ez Před rokem

      Mungu tenda miujiza kama ile.

    • @marialesulie6798
      @marialesulie6798 Před rokem

      What do know about better future? What do you know about investment?
      What do you know about business and contracts?
      What do you know? Nothing.
      It’s better to keep your mouth shut and learn some business issues before you comment here. Show your skills and knowledge.
      Show your love and patriotism to your country. Not just venders fats upepo. Do some homework before you say something in public. Conduct some critical analysis for your own benefit

    • @marialesulie6798
      @marialesulie6798 Před rokem

      @@PascalPascual-rn6fx wewe utafanikiwa? Kwa lipi?

    • @marialesulie6798
      @marialesulie6798 Před rokem

      Hujui ulisemalo pole sana

  • @user-su8yp7sc3e
    @user-su8yp7sc3e Před rokem

    Ungu atilinde juu ya majanga

  • @S.SWarfa
    @S.SWarfa Před 11 měsíci

    Vatican ni nani? Nyinyi maaskofu ndio munagawa wananchi. Munaogopa kuwa manaopata faida na bandari hamtapata tena.

  • @adamndoi2376
    @adamndoi2376 Před 11 měsíci

    Rc mko sawa Makanisa mengine na Waislamu Mbona hamtu tetei? (Bandali yetu)

  • @user-rc1dp6ux3k
    @user-rc1dp6ux3k Před 11 měsíci

    Kila anayeshabikia mkataba huu wana masilahi binafsi

  • @fransiskamwinuka4750
    @fransiskamwinuka4750 Před 11 měsíci

    Wakatoliki akili nyingi sana. Elimu imejaa kwa viongozi wetu. Hawabahatishi wanaposema jambo lao. Wanaona mbali sana. Mama Achana na hiyo hiashara haina issue. Sikia maneno ya wabobezi wa kila ki2. PHD zipo vichwani kwa hao maaskofu.
    Achana na hao wanaokuvika kilemba cha ukoka. Sikiliza maneno yenye busara kutoka kwa wasomi Maaskofu.

  • @adimudachi7984
    @adimudachi7984 Před rokem +1

    Kumbe vatcani ndo inaivuluganchi waingereza wanawapawaarabu nyinyi mnapinga kumberoma ndo wanakulanchi pekeyao da lakini poa putiniyupo somari wanaakili hawataki dhurma

    • @marialesulie6798
      @marialesulie6798 Před rokem

      Kama huna la kuongea nyamaza. Hujielewi

    • @annasolomon9855
      @annasolomon9855 Před rokem

      😂😂vjinga kubwa wew ndio maana unaandikia somaria badala ya somalia

  • @sharifakhalfan2475
    @sharifakhalfan2475 Před rokem +1

    Ingekuwa wazungu wacnge SEMA Ila kwa MWAARABU imekuwa balaa Allah tulinde. Cc pamoja na Dini yako INSHAALLAH

    • @marialesulie6798
      @marialesulie6798 Před rokem

      Tumia akili acha kuwa na mawazo finyu yasiyo na tija. Hii ni nchi yetu sote siyo ya wageni bali wazawa. Acha fikra potofu hutafika popote

    • @brendangabriel1643
      @brendangabriel1643 Před rokem

      Sisi hatuna shida na mwarabu wala mzungu, aje ye yote tu. Shida kwetu ni kilichoandikwa ndani ya mkataba, rekebisha uozo ulioko kwenye mkataba tu, kisha tusonge mbele. Hayo ya mwarabu au uislamu ni ya kwako na wenye akili kama zako. Sisi wazalendo wakiwemo TEC tunaangalia raslimali zetu kwa sasa na vizazi vijavyo, si vinginevyo.

    • @user-ze6bh9zv9s
      @user-ze6bh9zv9s Před 11 měsíci

      Tunaomba mushirikiane kama hivi kupinga ushoga na ulawiti tunataka kusikia kauli zenu maaskofu

  • @SanaiKiruki-db3nf
    @SanaiKiruki-db3nf Před rokem

    Kwa kuishauri wizara ya mipango na uwekezaji vizuri. Hekima ya Mungu imuongoze

  • @user-ih6yy3so5q
    @user-ih6yy3so5q Před rokem

    Watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi hii tuoo nyuma ya Mababa Askofu tunapinga kwa nguvu zote bandari kuuzwa kwa waarabu na pia KIA yetu je

    • @yahyadenny4368
      @yahyadenny4368 Před rokem

      unaunga mkono utumbo?wapi bandari imeuzwa?mmefundishwa utii wa woga ndo maana mnakubali kila kitu.biblia inasema mjinga hukubali kila lisemwalo.

  • @user-rc1dp6ux3k
    @user-rc1dp6ux3k Před 11 měsíci

    CCT TOENI TAMKO KMYA CHENU KINA MSHINDO

  • @kawiche4911
    @kawiche4911 Před 11 měsíci

    TANGANYIKA HATUTAKIBALI KUTOA BANDARI ZETU MKATABA UFUTWE HARAKA SANA

  • @kassimualli1755
    @kassimualli1755 Před rokem +2

    Nyie mnaopinga muda si mrefu mtaharisha kwa kuona uwekezaji unafanyika

    • @felistermedard9876
      @felistermedard9876 Před rokem

      Utaharisha wew

    • @fmbilinyi5137
      @fmbilinyi5137 Před rokem +2

      Kinachopingwa ni mkataba mbovu sio uwekezaji. Tupo tayari Dp world waje wawekeze ila hayo mashart ya mkataba yarekebishwe

    • @marialesulie6798
      @marialesulie6798 Před rokem

      @@fmbilinyi5137 hatuwataki dpw wameonesha nia mbaya na sisi.
      Wawekezeji waje lakini iwekwe tenda mezani washindaniehwe. Atakayekuja na manufaa zaidi achukuliwe. Bandari ni yetu wanaitamani wengi lazima turinge. Anayekuja afate masharti yetu. Tusiwe wanyonge

    • @marialesulie6798
      @marialesulie6798 Před rokem

      Hara wewe usiyejitambua. Huwezi kutafakari mambo akili yako inaonekana imeganda

    • @marialesulie6798
      @marialesulie6798 Před rokem +1

      Hujui moja na moja ni ngapi nahisi hata shule uilifeli wewe. Hata Kibarua cha kusafisha mbwa wao hawatakupa wewe labda kuzoa mavi yao

  • @user-gc1ez1yv4k
    @user-gc1ez1yv4k Před rokem

    Tanzanite ndiyo akina Msiba.Mmeingia mkenge Mtapigwa kila Kona.

  • @benson20301
    @benson20301 Před rokem +1

    Imefika huko tena jamani

  • @martinlaurence947
    @martinlaurence947 Před rokem

    Mfumo wa uundaji wa serikali unakasoro na ndo maana watu hawasomi mikataba kwa kuwa wengi wao elimu Yao ni ndogo, pia jk asijihusishe na uongozi uliopo madarani

  • @husseinkassimu2714
    @husseinkassimu2714 Před rokem +1

    Waache unafki wajibu hoja za mzee waupako mbona swala laushoga hawakutoa waraka inamana mungu karuhusu ushoga watawadanganya hao hao uliogubikwa na giza kanisa ndio chombo kinachoongoza kua na taasisi zinazoingiza bizaa sawa nabure inch hii mtawadanganya wajinga ndio maana hata mwendazake mlimchukia alivyo anza kuwabana wa wadini kuhusiana na vitu wanavyo ingiza inchni

    • @angelashitindi5427
      @angelashitindi5427 Před rokem

      Kwani kuna mkataba wa ushoka ulioletwa inchini kwetu, TEC ina wasomi mjomba hawakurupuki

  • @Focusm-se2sd
    @Focusm-se2sd Před rokem

    Ni kweli ccm imeshindwa kuongaza nchi yetu tunaungana na maaskofu wetu

  • @abdallahally842
    @abdallahally842 Před rokem +3

    Mko kwa maslahi ya vatican roma italy na sio maslahi ya watanzania. Kanisa la wataliano halijawahi kua na maslahi na watanzania kuanzia kupigania uhuru halikutaka wazungu waondolewe na liko kwa msalahi ya kuiba na kuhodhi ardhi yawatanzania kutorosha madini kutokulipa kodi bandarini liko kwa maslahi ya vatican na sio ya watanzania hilo liko wazi

    • @explorewithbertin
      @explorewithbertin Před rokem

      Jibu hoja zilizo kwenye mkataba achana na walioleta hoja maana hao ndo viongozi wa waumini waliowengi nchi hii

    • @marialesulie6798
      @marialesulie6798 Před rokem

      Kama huna hoja ya maana bora unyamaze maana unaonekana mjinga.
      Hapa tuko kutetea bandari zetu zisiuwe kwa wageni full stop. Hayo mengine ni yako kaa nayo.
      Bandari zetu hazimilikishwi popote ni mali yetu halali na urithi wetu tuliopewa na Mungu full stop.
      Umbea hatutaki usitutoe kwenye reli.

    • @marialesulie6798
      @marialesulie6798 Před rokem

      @@explorewithbertin hujitambui huyo

    • @rosetreffert4179
      @rosetreffert4179 Před rokem

      ​@@marialesulie6798kabisaa !@mijutu mingine vilaza mambo ya muhimu wanafanya ushabiki

    • @floramongi1410
      @floramongi1410 Před rokem

      Abdallah may be you are true

  • @CanonLuhunga-oc9sx
    @CanonLuhunga-oc9sx Před rokem

    TEC,Askofu Kilaini anasemaje

  • @HumphreyNoah-yx8jf
    @HumphreyNoah-yx8jf Před rokem

    Good

  • @gordfreysangawe7535
    @gordfreysangawe7535 Před rokem +1

    Kuna nini hapa bandarini tangu lini maskofu wamekuwa watetezi wetu? Sisi wakist walituoji lini Hadi waseme hatutaki mkataba amba hata Sisi atujui ni nini hicho kiukwe kutakuwa na watu walikuwa wanafaidika na hii bandari sasa hawataki uwekezaji huu tutawajua wote endeleeni kujitokeza tuwajue acheni kujishika na wananchi Sisi hatujawatuma MTU zaid ya serikali yetu

    • @theodorythobius3965
      @theodorythobius3965 Před rokem

      Sisi na nani? Mimi ni mkristo na naupinga mkataba wenye vipengele vya kulinyonya taifa.
      #viongozi wa dini ni wawakilishi wa waamini wao.
      @gordfreysangawe, hebu tafuta muda uupitie mkataba kwa namna yoyote kabla ya kujaku-comment.

    • @iddyjohn1032
      @iddyjohn1032 Před rokem

      ​@@theodorythobius3965kama unao h3mbu nitumie na mimi,alafu hiyo wengi hawataki mmepata wapi????
      Mimi binafsi nahitaji bandari ipate muwekezaji lakini maslahi ya taifa yatizamwe vyema ,sasa kwanini nyinyi mnasema uvunjwe tu ,why uvunjweeeeee??haya na vatcan ina mmalaka gani ya kuingilia mambo ya ndani ya nchini isio kuwaa ya kwao,wanapata wapi jeuri???mbona wakristo ndio mnachokochoko sana,na serikali imewapa nafasi ya kutoa maoni iweje ?? lakini mmeeenda mbali sana sana sana

    • @iddyjohn1032
      @iddyjohn1032 Před rokem

      Mwaka 1992 hawa hawa waliing ia mkataba na serikali ili wapate fedha kutoka serikalini kodi za watanzania waendeleze shule za na hospitali zao ajabu ukiacha kubwa ni mkataba mbovu na unanyonya jamii fulani lakini hayo mahospitali ndy kwanza yana gharama kuliko hata za serikali na ilihali wanapata fedha kibao,Kcmc inawahudumu mpka leo wanalipwa na serikali lakini huduma ziko juu,saasa kama hawa ni watetezi wa wananchi kweli vipi waliingia mkataba wa kunyonya jamii fulani???na mbona ukawa kimya kimya???

    • @kiatu
      @kiatu Před rokem

      Umepewa nini ndugu?

    • @brendangabriel1643
      @brendangabriel1643 Před rokem

      ​@@iddyjohn1032Hujui unachoandika hapa, bora ukae kimya. Hospital na shule za kanisa ndio mkombozi mkubwa ktk maeneo mengi nchi hii kuliko za serkali kabla na baada ya uhuru mpaka leo. Umezaliwa lini wewe hayo huyajui? Je ulitaka utibiwe bure? Hata hivyo, zina gharama nafuu kuliko zingine.

  • @user-dw3my3xp4d
    @user-dw3my3xp4d Před rokem

    Tunaingia kwenye ukolon kama miaka yote tunao leo tunabadilixhwa kwenye ukolon

  • @babuloliondo74
    @babuloliondo74 Před rokem +1

    Waisraam tunautaka tenasana amna mtu atatuzuiya mkataba wabandari bandari mnabebea mitumba kutoka china

    • @janetmutashubilwa3041
      @janetmutashubilwa3041 Před rokem +1

      Basi nyie waislamu mu upeleke Zanzibar kwenye uislamu wenu Tanzania Ina wakristo

    • @babuloliondo74
      @babuloliondo74 Před rokem

      @@janetmutashubilwa3041 wewe jiongopee tanzania wakristo na waisraam wengi wapi angaria sensa wewe kweri usingizi

    • @babuloliondo74
      @babuloliondo74 Před rokem

      @@janetmutashubilwa3041 mtapiga kerere adi makanisani mtaimba mpaka midomo ipasuke mkataba afutwi

    • @user-cz7bd9tc5k
      @user-cz7bd9tc5k Před rokem

      MA Askovu kazi Mume Ifanya vema piteni kama Mupanzi Wakishupaza shingo Muwa Ache wafanye watakavyo Tuli chagua vipofu Watu ongoze Mkatwambia chaguo la MUNGU Sasa Muna lalamika nini?Kumbukeni Hayo ni Mapenzi ya MUNGU Mali Za Dunia ni Za Watu wote Waliopo Duniani Hata DPW Wana haki MUNGU Hana Mpaka

    • @sabraham5308
      @sabraham5308 Před rokem

      @@janetmutashubilwa3041Tanganyika waislamu ni asiimia 65%,wakristo 30%

  • @NdeshaPaul-uz9bw
    @NdeshaPaul-uz9bw Před 11 měsíci

    Pumbs u kuliko upumbavu wenyewe.hata huyio mwarabu hatakutambua hata kukupa makombo yake. Subiri uone utajits sana. Kama wewe ni fungu la waislamu kwa nini asikutambue sasa? Hakutambui wala hatajua kama kuna mtu kama wewe uliyekuwa unang'anania mkakataba usioijia. Mpimbavu ana asili ya upumbavu ni kazi bure kimfundisha hafundishiki kamwe.

  • @abujamalaalghammawiy7470

    Hao TEC (WAKATOLIKI) ndio wauwaji na wanaochochea mauwaji katika nchi nyingi za kiafrika. Mauwaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 kanisa katoliki limehusika moja kwa moja katika mkauwaji ya waafrika.
    Hilo kanisa limalipwa na wazungu, ndiomaana hawana uchungu na amani ya nchi yetu, maana wao wanajua nchi ikitokea vita, wao watakimbilia Vatcan wakakae kwa starehe. Sisi ndioo tutabaki tunaangamia

  • @mawazoselemani614
    @mawazoselemani614 Před rokem +4

    Miaka sita ya mwamba kalotengeza taifa miaka miwili keshalibomoa😂

  • @sadallahbataza1906
    @sadallahbataza1906 Před rokem

    Mimi nalia na bunge tu linamuwakilisha nani bungeni? Serikali au wananchi? Kwanini wametusariti kiasi hiki? Wasitake tuamini walichaguliwa kimagumashi na si ridhaa yetu

  • @zainabumartin9520
    @zainabumartin9520 Před rokem

    😅

  • @MichaelLigi
    @MichaelLigi Před rokem

    Hatutaki mkataba wa bandari yetu kwani tokea

  • @mwitamarwa329
    @mwitamarwa329 Před rokem

    Let us not take for granted the peace we in Tanzania