NGOMA YA KINYAKYUSA "Mang'oma" (kehtuli-Ngeleka)

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 27. 11. 2022
  • #TraditionalDance
    #Nyakyusa
    #Wanyakyusa
    Mang'oma ni ngoma maarufu ya utamaduni wa Wanyakyusa.
    Ngoma hii huchezwa baada ya mavuno ya Mpunga na kipindi ambacho ndizi zinakuwa zimekomaa sana kwaajili ya chakula.
    kwa zamani, kila eneo lenye Chifu lilikuwa pia na ngoma yake ambayo inamtindo wake wa upigwaji na uchezwaji, ukiwa unatafsiri yake.
    Ngoma hii ya ing'oma huwa na malengo yake ambayo huwa ni Kudumisha umoja, Kuburudisha, Kuelimisha, Kudumisha Mila na Kutoa uwanja wa biashara.
    Ngoma hii ili ikamilike huwa na timu tano. Hizi timu huwajibika kwa mtindo wao na kazi yao maalumu ya kuchangiza kwatika kufanikisha kitoa burudani husika.
    Ngoma huwa na timu ya Wazee waongoza ngoma, Mpiga ngoma kubwa, Wacheza Stepu na Fimbo, Wapiga ngoma ndogo ndogo, Wapiga vivvuzela, Wacheza step bila fimbo.
    Katika michezo hii ya ing'oma ambayo hujumuisha ngoma kadhaa kutoka mahala mbalimbali ambazo zinakuwa zimealikwa kushiriki, huwa pia kunakumtafuta mshindi ambako hufanywa haswa na mashabiki, ambao huwa na jukumu kujua ni ngoma ipi imeongoza katika mwaliko huo.

Komentáře • 10