REKODI MPYA BANDARI YA DSM, MELI KUBWA ILIYOBEBA MAGARI 4,041 KUTOKA JAPAN YATIA NANGA

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 11. 09. 2024
  • REKODI MPYA BANDARI YA DSM, MELI KUBWA ILIYOBEBA MAGARI 4,041 KUTOKA JAPAN YATIA NANGA
    Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, ameagiza Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kuanza kutumia Bandari Kavu zinazokidhi vigezo pamoja na kupunguza idadi ya siku za kushusha mizigo ili kupunguza msongamano wa magari na mizigo katika bandari Kuu ya Dar es Salaam.
    Waziri Profesa Mbarawa ametoa agizo hilo leo wakati wa mapokezi ya meli kubwa yenye urefu wa mita 189.45 ikiwa na shehena ya magari 4,041 kutokea nchini Japan, ambapo magari 2,936 kati ya hayo, yanasafirishwa kuelekea nchi zingine huku mengine 1,105 yakisalia Tanzania.
    Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamkala ya Bandari Tanzania (TPA), Erick Hamisi amesema ujio wa meli hiyo, ni matunda ya maboresho yaliyofanyika katika bandari Kuu ya Dar es Salaam.
    Itakumbukwa, Agosti 10, 2021 kabla ya ujio wa shehena hiyo, Mamlaka ya Bandari Tanzania ( TPA) iliandika historia ya kwanza kupokea shehena kubwa ya magari tangu kuanzishwa kwa bandari hiyo, baada ya meli kubwa ya kubeba magari, kutia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam ikiwa na magari 3,743.
    @hamisimguta

Komentáře • 35

  • @olenyghosho7008
    @olenyghosho7008 Před 2 lety +3

    RIP jpm

  • @pendorichard2630
    @pendorichard2630 Před 2 lety

    Waoh

  • @peterbaton6501
    @peterbaton6501 Před 2 lety +2

    Ndio Story Zilixo baki

  • @natafutapesa9678
    @natafutapesa9678 Před 2 lety +1

    Sasa mbona tunaendelea kua nchi masikini? Wizi tu yani hadi mnakera

  • @yusuphalexander7727
    @yusuphalexander7727 Před 2 lety

    hivi kweri tunania njema kama tunashangilia lekodi imewekwa

  • @godsonndamgoba8053
    @godsonndamgoba8053 Před 2 lety

    Hiv kwa kusema ni record ,inasaidia nn

  • @hamzamoshi8275
    @hamzamoshi8275 Před 2 lety

    Kwaiyo inamaana zamani walikuwa hawaibi mabosi hapo bandari bali walikuwa wanafanya kufuru ya wizi 🤔

  • @mwanagwakyala3213
    @mwanagwakyala3213 Před 2 lety

    Ahsante Magufuli .

  • @HusseinRj
    @HusseinRj Před 2 lety +3

    Mafuta wanayo?

  • @jeffkonki8279
    @jeffkonki8279 Před 2 lety +1

    Magari kibao ya jirani ushuru unaenda wapi ? Mavitu mnatupandishia bei juu

  • @athumanmkilindi6215
    @athumanmkilindi6215 Před 2 lety

    Nchi ya ovyoo kwel

  • @Worldunite
    @Worldunite Před 2 lety +1

    ..yaani bila ya kuwepo mtu mweupe pichani ina maana hatuwezi kuendesha shughuli zetu sisi wenyewe????

    • @kiri5807
      @kiri5807 Před 2 lety

      Inaonekana unachuki mno na watu weupe . Nenda ukamuondoshe ukaye wewe basi .

  • @abedomar5183
    @abedomar5183 Před 2 lety +2

    RIP Magufuli

  • @annrobin9291
    @annrobin9291 Před 2 lety

    Nikajua imebeba mafuta

  • @yusupramadhani4427
    @yusupramadhani4427 Před 2 lety

    Langu mojalipo apooo

  • @pendorichard2630
    @pendorichard2630 Před 2 lety

    Sasa pesa mnapeleka wapi nchi masikini mpaka huruma

  • @hakimsashamusic
    @hakimsashamusic Před 2 lety

    Play don't worry by hakim sasha

  • @georgemhalla8853
    @georgemhalla8853 Před 2 lety

    Kila kitu Rais Rais Rais Rais, not good at all

  • @elishaelisha6755
    @elishaelisha6755 Před 2 lety

    Wiz mtupu

  • @Worldunite
    @Worldunite Před 2 lety

    Kila rais amechangia, msiwapange kwa madaraja jmn

  • @zahorosuleiman1099
    @zahorosuleiman1099 Před 2 lety

    Mhh

  • @Muhsmart
    @Muhsmart Před 2 lety

    😂😂😂 yani katika magari elf4000 ya bongo buku asa si bora bandari tu isiwe yetu tu

    • @welcometoeat165
      @welcometoeat165 Před 2 lety

      Sasa hapa s meli imepita tu love! Inashusha mzigo afu inasepa zake

    • @kondoatown8765
      @kondoatown8765 Před 2 lety +1

      Yanashuka magari 4000 yote tunakula ushuru wake kwetu Tanzania 🇹🇿 Kisha yaende huko kwao sisi tushabaki na pesa .

    • @kiri5807
      @kiri5807 Před 2 lety

      Wewe unajua hiyo meli kupita tu inalipa ushuru wa bandari kiasi gani ?

    • @Muhsmart
      @Muhsmart Před 2 lety

      @@kondoatown8765 bandari yetu ila nchi zinazotumia iyo bandari sio sisi Tz asa kuna uhumn gani sis tunbaki na ushuru wenzetu awana bandari ila wnaingiza pato kubwa kuliko sisi wenye bandari mfno uganda, zambia

    • @Muhsmart
      @Muhsmart Před 2 lety

      @@kiri5807 yeah kwa apo ni swa tufanye kas ya elf 10000 afu sisi tulipwe 100 pato wanalotoa apo ni dogo compared tu uko kwao ila ssi tunaona hela mingi