KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA YATATUA MIGOGORO YA WANANCHI LUDEWA

Sdílet
Vložit
  • čas přidán 7. 09. 2024
  • MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN YAENDELEA KUSAIDIA WANANCHI WA LUDEWA
    Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) Wilayani Ludewa, katika Kata ya Madilu ambapo wananchi wameendelea kupata elimu ya Masuala ya kisheria kwenye ardhi, madai, mirathi, ndoa, jinai, haki za binadamu, utawala bora na utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala.
    Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mkuu wa Wilaya hiyo ya Ludewa Mhe. Victoria Mwanviza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan; kwa kampeni hiyo ya Kitaifa ambayo Wataalam wa Sheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wapo wilayani hapo kusaidia wananchi kupata huduma hiyo.
    Kampeni hiyo pia imesaidia wananchi hao kupata huduma ya msaada wa Kisheria kwa haraka, kusaidia uwakilishi wa wananchi wasio na uwezo Mahakamani, kujenga uwezo kwa mabaraza ya usuluhishi ya Kata na kujenga uwezo kwa Watumishi wa Serikali ngazi ya vijiji na Kata.

Komentáře •